DC CHONJO APOKEA MABATI M100 KUTOKA KAMPUNI YA UJENZI NANDHRA.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, (kulia) akipokea Mabati yaliyotolewa na Kampuni ya Ujenzi ya Nandhra. |
Mabati yaliyotolewa na Kampuni ya Nandhra. |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa mabati. |
MKUU wa
Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amepokea Mabati 100 kutoka katika
Kampuni ya Ujenzi ya Nandhra inayosimamia miradi mikubwa ya Kimkakati Manispaa ya Morogoro ikiwamo Ujenzi wa Soko
Kuu la Kisasa pamoja na Stendi Mpya ya Daladala.
Tukio
hilo la kukabidhiwa Mabati hayo
limefanyika leo Mei 28, 2020 nje ya Ofisi yake .
Akizungumza
na Waandishi wa habari , ameishukuru Kampuni hiyo kwa msaada walioutoa huku akiziomba Kampuni nyengine za Ujenzi zilizopo Manispaa
ya Morogoro pamoja na Wilaya ya Morogoro, waweze na wenye we kurudisha kidogo
ile asilimia wanayopata kwa ajili ya maendeleeo ya Wananchi wa Morogoro.
“Tunashukuru
kwa mchango wenu, tunashukuru kwa kuwa mnatambua thamani ya elimu ndio maana
mkaona msaidie Mabati kwa ajili ya Shule zetu , hata nyie kama msingepata elimu
hata hivyo vigezo vya kuwa wakandarasi msingevipata, na hata katika uombaji wa
tenda lazima ueleze vigezo na utaalamu wako lakini utaalamu huo huo umetokana
na kupata elimu, nawashukuru sana naamini mchango huu utakwenda kufanya kazi
kama ilivyoelekezwa na nyie mtaiyona yenye manufaa katika Manispaa yetu’’
Amesema DC Chonjo.
Aidha,
amesema katika Mabati 100 waliyokabidhiwa, Mabati 50 watayaelekeza katika Shule
ya Msingi Mji Mkuu kama mkopo ili yaendeleze ujenzi na watakapopewa mabati yao
watayarudisha kwa ajili ya kuelekeza
katika Shule nyengine.
“”Mkurugenzi
nakukabidhi Mabati haya 100, Mabati 50 tuwakopeshe Shule ya Msingi Mji Mkuu
maana kuna ahadi nyengine ya Mhe. MNEC
wa Taifa Hassan Bantu ambaye aliahidi Mabati 50 katika Shule hiyo, lengo
la kuwakopesha ni kwamba haya tunayowapa yakamalizie ile kazi na atakapo yaleta
hayo 50 aliyoyaahidi mwisho wa mwezi huu tutayarejesha ili Shule nyengine zenye
matatizo mfano Shule ya Kihonda nimeambiwa inavuja hivyo yaelekezwe huko kwa
idadi ambayo itamaliza matatizo na yatakayobakia mtaangalia shule nyengine
zenye matatizo au Zahanati “ Ameongeza DC Chonjo.
Hata
hivyo, ametoa rai kwa Wananchi wa Morogoro kwamba waanzishe miradi katika
maeneo yao na hatua ambazo watafikia Uongozi wa Wilaya , Manispaa na Wadau
wengine wa maendeleo watasaidia.
Katika
hatua nyengine ,amewaomba Watendaji wa Kata kuendelea na Zoezi la kuongeza
Madarasa na wale watakaonza ujenzi huo mfano Diwani au Mtendaji atayesema
tayari ameanzisha basi Uongozi wa Wilaya na Manispaa utakuwa na jukumu la
kumalizia.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, ameishukuru
Kampuni ya Ujenzi wa Nandhra ambao ndio Mkandarasi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa
Soko Kuu la Kisasa, Stendi mpya ya Daladala pamoja na Stendi ya Kaloleni kwa
mchango wao wa Mabati kwa jili ya manufaa ya Morogoro na Sekta ya Elimu kwa
ujumla.
“
Tunawashukuru kwa Mabati ambayo mmetupatia ambayo yatakwenda kusaidia kwenye
shule zetu, kuna ambazo ni kongwe ambazo baadhi zinavuja lakini pia kuna shule
ambazo tunazifufua , lakini shukrani zaidi zimuendee Mbunge wetu wa Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz
Abood kwa jihudi zake za kuwa karibu na wananchi wake na kutusaidia kwa vitu
mbalimbali katika Manispaa yetu ya Morogoro ‘’Amesema Lukuba.
Lukuba
,amewaomba wadau wengine wa maendeleo wanaoguswa na masuala mazima ya elimu ,
afya katika Manispaa ya Morogoro waendelee kujitokeza na kutoa misaada zaidi na
kuunga mkono juhudi zinazofanya na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli
Naye
Msimamizi wa Mradi wa Soko Kuu la Kisasa Morogoro, Eng. Charles Richard,
amesema wametoa mabati hayo kwa ajili ya kuunga mkono Sekta ya elimu ambayo
imekuwa ikipewa kipaumbele na Mhe. Rais
Dkt John Magufuli kwa ajili ya kuisogeza sekta mbele kwa maendeleo ya Taifa kwa
ujumla.
“Tunakuhakikishia
Mkuu wa Wilaya kwamba hiki tulichotoa itakuwa sio mwisho tutaendelea
kushirikiana ili tuweze kurudisha kwa jamii asilimia zitakazo kwenda kufanya
shughuli nyengine, lengo ni kuhakikisha Sekta ya elimu inakuwa na inafanikiwa”
Amesema Eng. Charles.
Post a Comment