DC Chonjo athibitisha kuingia kwa Tani 90 za Sukari Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, akiwa Ofisini kwake akizungumza na Waandishi wa habari juu ya kuwasili kwa tani 90 za Sukari. |
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo,
amethibitisha kuingia kwa Sukari tani 90 kufuatia kupanda kwa bei ya sukari
katika Wialaya ya Morogoro.
Hayo ameyazungumza leo Mei 11, 2020 Ofisini kwake katika
kikao cha waandishi wa habari juu ya suala la kupanda kwa bei ya Sukari katika
Wilaya ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari, DC Chonjo, amesema suala
la Sukari limekuwa changamoto sana na sio Wilaya ya Morogoro hata Mkoa Mzima wa
Morogoro sukari imekuwa tatizo.
Chonjo, amesema kupanda kwa sukari kumetokana na baadhi ya
wafanyabiashara kuuza bei ya Sukari kinyume na bei elekezi ya Sukari iliyotolewa kupitia Bodo ya Sukari Tanzania.
Amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa kushusha tani 90 kwa
wafanyabiashara wakubwa ambapo wafanyabaishara hao wataisambaza sukari hiyo kwa
wafanyabaishara wa nusu jumla kwa kufuata utaratibu ambao Serikali imeuweka.
“Upatikanaji wa Sukari hapa Wilaya ya Morogoro umekuwa changamoto
kidogo, lakini sio Wilaya ya Morogoro tu na mkoa mazima pia , niishukuru
Serikali ya Jamhuri hii ya awamu ya inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwa sikivu imeendela kutoa
vibali ili tuweze kuagiza Sukari kutoka nje, na leo tumepokea Sukari tani 90
ambapo mgao wake utatolewa kwa wafanyabiashara wa jumla “ Amesema DC Chonjo.
Aidha amesema miongoni mwa wafanyabiashara wajumla ambao wamegawia Sukari
hiyo kwa ajili ya kusambaza,ni pamoja na Sadiki amepata tani 30, Binzoo tani
30na Digamba tani 30.
Amesema Sukari hiyo itagaiwa kwa Mkoa mzima wa Morogoro na
sio kwa Wilaya ya Morogoro peke yake
Amesema katika ugawaji huo kutokana na magari makubwa
hayaruhusiwi kuingia mjini, hivyo ugawaji wake utafanyika maeneo ya maegesho ya magari
Nane nane kwa kuwakabidhi wafanyabishara wa jumla tu ambapo baada ya hapo wale
wajumla watasambaza kwa wafanyabiashara wa nusu jumla kwenye maduka yao ili kuepusha msongamano wa
watu hususani katika kipindi hiki cha mapambano dhid ya Ugonjwa wa CORONA.
Kuhusu bei elekezi, Chonjo, amesema kwa wafanyabiashara wa
jumla watatakiwa kuuza sukari hiyo kwa mfuko mmoja wa Kilo 50 kwa shilingi 127,000/=
, kwa wale wanusu jumla watauza kwa shilingi 128,000/=na wale wa
wafanyabiashara wa reja reja watatakiuwa
kuuza kilo moja kwa shilingi 2,700/= kama bei elekezi inavyotaka.
Amesema wale watakao kiuka bei elekezi watachukuliwa hatua
kali za kisheria ikiwamo kuwapa kesi ya uhujumu uchumi kwa kutakataa na kukiuka
maagizo ya Serikali.
Mwisho amewaomba Wananchi wa Wilaya ya Morogoro kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito kwani suala la sukari litamalizika na
kila mwananchi atanufaika na huduma hiyo na kurudi kama zamani kwani hata
sukari iliyoletwa haiwezi kukidhi kwa maeneo yote hivyo wanatarajia kupokea
tani nyeninge za siukari kutoka Serikalini.
Post a Comment