Meya Manispaa ya Morogoro awakalia kooni wakandarasi wasio na sifa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, (kushoto) akipewa maelekezo na Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro Eng. Juma Gwisu wakati wa kukagua ujenzi wa Stendi ya Daladala Kaloleni.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga,(mbele ) akimuelekeza jambo Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro Eng. Juma Gwisu katika eneo la mradi wa Ujenzi wa Stendi Kaloleni.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kuzungushia uzio katika Ujenzi wa Stendi ya Daladala Kaloleni. |
Eneo la Ujenzi wa Stendi ya Kaloleni linavyoonekana baada ya kuzungusha Uzio. |
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya
Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, amepiga marufuku wakandarasi wasio na sifa kuomba kazi katika Manispaa ya Morogroro.
Hayo ameyasema leo Mei 5, 2020 mara baada ya kutembelea na
kukagua mradi wa Ujenzi wa Stendi ya Daladala ya Kaloleni unaoendelea kufuatia Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kuvunja
mkataba na Mkandarasi Kampuni ya Fast na kukabidhi mradi huo kwa mkandarasi
mpya kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Nandhra.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Kihanga, amesema Wakandarasi wasio nasifa marufuku kuomba kazi
Manispaa ya Morogoro na wakigundulika
wamepatiwa kazi na wakashindwa kutekeleza kwa wakati watapata hasara zaidi ya
kile walichokiomba.
“Leo nimeona nipite kuangalia ujenzi huu wa Stendi ya
Kaloleni , wiki iliyopita katika Kikao cha Baraza Mkurugenzi wa Manispaa
alitueleza kwamba washavunja mkataba na Mkandarasi wa zamani na wamekabidhi
mradi huo kwa mkandarasi mpya ambaye ndiye anayeendelea na ujenzi wa Soko Kuu
pamoja na Stendi Mpya ya Daladala, nimeona kazi za kusafisha zimeanza tofauti
na ilivyokuwa mwanzo, matarajio yangu anaweza kwenda na muda kama tulivyoshauri
kwenye Baraza, nafikiri ilitumika busara kumpa mkandarasi huyu mradi kwani muda
uliobakia ni mdogo isingewezekana kuanza
kutafuta mkandarasi mpya, Ombi langu kwa Mkandarasi tufanaye kazi na tumalize
kwa wakati kwani fedha hizi tulizopewa kutoka ULGSP muda wake unakwisha Juni 30
mwaka huu 2020, ambapo tukishindwa fedha hizi zitarudi zilipotoka" Amesema Kihanga.
Aidha amemtaka Mkandarasi
kwenda na wakati kwa kipindi hiki cha miezi miwili waliyopewa
wahakikishe kwamba Stendi hiyo inaanza kutumika kwani waliwaondoa wananchi
katika eneo hilo wakiwa na matumaini ya kupata Stendi mpya yenye ubora licha ya
kutokea ukwamishaji uliojitokeza kutoka
kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Fast.
Amesema matarajio yake mradi huo utamalizika vizuri ili
Wananchi waliokuwa wakinufaika na huduma hiyo ya Stendi waweze kupata huduma
kama kawaida yenye ubora kwa wasafiri na kuwa moja ya Chanzo chengine cha Mapao
ya ndani katika Manispaa.
Hata hivyo amelaani vikali Wakandarasi wasio nasifa kupokea
fedha za ujenzi wakati wakijua hawana uwezo wa kujenga huku akimuomba
Mkurugenzi wa Manispaa kufuatilia ili
kuhakikissha fedha zote ambazo Mkandarasi wa Fast alizichukua zinarudi.
“Kumekuwa na maswali mengi watu wakijuliza hususani hawa
wenzetu wa daladala ambao tuliwahamisha eneo hili kupisha mradi lakini
mategemeo yetu yalikuwa ni mazuri kukamilisha mradi huu kwa wakati , kwahiyo
nalaani sana wakandarasi wanaomba kazi huku hawana uwezo, mbali na kupewa
advance ya Shilingi Milioni 100 lakini bado walishindwa kufanya kazi , lakini
ni wahahakikishie hizi ni pesa za Serikali zitarudi na sheria itafuata mkondo
wake, namtaka Mkandarasi amalize kazi hii kwa wakati kama tulivyokubaliana
katika Mkataba akichelewa mpaka ikafika mwezi wa 6, 2020 hizi fedha hazitakuwa
za kwetu “ Ameongeza Kihanga.
Hata hivyo ameendelea kutoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuendelea kufuata ushauri wa Wataalamu wa Afya katika kujikinga na Ugonjwa wa Corona ikiwemo kunawa Maji tiririka na sabuni, kutumia Vitakasa mikono ( Sanitizer), pamoja na kuepuka msongamano isiyo ya lazima na kukaa nyumbani kama mtu hana sababu ya Msingi ya kutoka
Kwa upande wa Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng. Juma
Gwisu, amesema kwa sasa Mkandarasi yupo site na baadhi ya Malighafi tayari
yameashaanzawa kutengenezwa na ameshasafisha eneo kwahiyo anaimani kazi itafanyika
vizuri .
“Kama unavyoona Mkandarasi wetu ameanza kwa kasi kubwa , Yule wanyuma
tulishavunja makataba naye na sheria zote tulifuata, lakini katika Ujenzi huu
tutajenga Choo cha kisasa ambacho kitazingatia watu wenye ulemavu lakini zaidi
hata Ofisi ya Kata tutaiboresha ili iendande na ubora wa Stendi” Amesema Gwisu.
Gwisu amesema kuvunja mkataba na Mkandarasi wa Kampuni ya
Fast kumetokana na Mkandarasi huyo kushindwa kufuata masharti ya mkataba wake
ya kukamilisha Ujenzi wa mradi huo wa Ujenzi wa Stendi ya Daladala Kaloleni.
Post a Comment