MANISPAA YA MOROGORO YAANZA UTOAJI WA TUZO ZA USAFI KATA NA MITAA.
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Morogoro , Samwel Subbi,akiunguruma na Redio Sauti ya Uzima juu ya maandalizi ya tuzo kwa Kata na Mitaa itakayofanya vizuri kwa usafi. |
Afisa Tarafa wa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako, akizungumza katika kituo cha Redio Sauti ya Uzima juu ya Kampeni ya Mazingira Manispaa ya Morogoro. |
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro ipo mbioni kuanza zoezi la utoaji wa tuzo za Usafi kwa Kata na Mitaa itakayofanya vizuri.
Akizungumzia
juu ya tuzo hizo,Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya
Morogoro , Samwel Subbi, amesema
wameamua kushindanisha Kata na Mitaa lengo likiwa kuweka Manispaa safi na
kuleta hamasa kwa Watendaji wa Kata pamoja na Mitaa.
Amesema Moja ya matarajio makubwa ambayo
yataleta mafanikio katika Kampeni ya Usafi ni pamoja na Viongozi wa Halmashauri
kushawishi wananchi wake kuchangia ada ya taka kwa ajili ya ukusanyaji na
uzoaji taka katika ngazi ya kata na Mitaa kwa ujumla.
Subi, amesema , mashindano hayo kwa upande wa ngazi ya Kata yatasimamiwa na maafisa afya na watendaji yakilenga kusimamia zaidi masuala ya usafi na utunzaji wa Mazingira
pamoja na jinsi ya kugeuza taka kuwa mali.
Amesema kuwa katika mashindano hayo vitatumika
vigezo na mashindandano ambapo kwa kila robo mwaka mashindano hayo yatafanyika na
matokeo yake kuwasilishwa katika Baraza la Madiwani .
Vigezo vitakavyotumika ni pamoja na udhibiti
wa taka ngumu, usafi wa barabara, mifereji, maeneo ya wazi, stendi za daladala, udhibiti wa taka maji, usafi wa
Masoko na Magenge, usafi wa Majengo ya biashara,usafi wa Taasisi, upendezeshaji
wa Mazingira, udhibiti wa uzururaji wa wanyama, uwepo wa vyoo bora, udhibiti wa
shughuli za uchafu na uharibifu wa Mazingira, usafi wa maeneo ya makaburi
pamoja na udhibiti wa Kilimo cha mazao marefu katikati ya Mji.
“Baada ya uzinduzi wa Kampeni yetu ya Usafi ,
sasa tumeona ili tuweze kufanikiwa zaidi tutoe zawadi kama motisha kwa Kata na
Mitaa itakayofanya vizuri, lakini sio tu tuzo tutatoa fomu zitakazojazwa na Maafisa wa Afya wa Kata
jinsi walivyoshughulikia changamoto ya uchafu katika maeneo yao na fomu hizo
zitawasilishwa kwa Afisa Mtendaji kabla ya kufika Manispaa kwa ajili ya
ufuatiliaji, tunawaomba Watendaji , Maafisa afya , pamoja na Wananchi
tushirikiane kikamilifu ili Kampeni yetu iweze kufanikiwa hatimaye na sisi
Manispaa siku moja zije Manispaa nyengine kujifunza kwetu “ Amesema Subbi.
Amesema zawadi hizo zinatarjiwa kutolewa siku
ya kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani , hivyo Watendaji wote kwa kushirikiana na Maafisa afya wanatakiwa
kuwasilisha taarifa za Mitaa iliyofanya vizuri katika Kata zao ili timu ya
Mazingira iweze kuzipitia na kuwapata washindi.
Katika hatua nyengine,amewaomba Maafisa
Watendaji kushirikiana kikamilifu katika kuzuia katazo la Vifungashio vya
palstiki ambavyo Serikali imepiga marufuku.
“”Kuanzia tarehe 1- hadi 15 mwezi Juni, 2020
tunaomba tuwasilishiwe taarifa Manispaa kwa Mitaa yote iliyofanya vizuri katika
Kata, na sisi kuanzia tarehe 15 -25 mwezi Juni, timu yetu ya Wataalamu wataanza
mchakato wa kuchuja na kuwapata washindi, ambapo washindi hao Kata zitatoka 3
na Mitaa 3, lakini suala zima la zawadi limebakia kwenye Kamati
tutakapokamilisha mipango yote tutazitaja zawadi hizo” Ameongeza Subbi.
Kwa upande wa Afisa Tarafa wa Manispaa ya
Morogoro, Winfred Kipako, ambaye ndiye katibu wa Kampeni ya usafi, amewaagiza
Watendaji wa Kata kuwaelekeza Maafisa afya jinsi ya kuandaa mpango kazi katika
Kata zao ili iwe rahisi kwa ajili ya ufuatiliaji.
Kipako, amesema tayari kuna wakuu wa Kanda za
Kampeni ya usafi wameshapangwa na kilichobakia wanasuburia barua rasmi kutoka
kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ili kuzishusha kwa watendaji waweze
kuwafahamu na kushirikiana.
“”Tumejipanga vizuri, tangu tuanze Kampeni
yetu kwa mara ya pili hii tumeanza katika Shule ya Msingi Mafisa A Kata ya Mwembesongo na Kata ya Mji Mkuu , tumeona kuna mwanga, nimeshuhudia baadhi ya maeneo
yameanza kuimarika na yanaleta taswira nzuri sana, bado kuna changamoto ya wale
wenye maeneo ambayo hawayaendelezi kuwa vichaka, tunatoa tamko wayafanyie usafi
mara moja zaidi wakishindwa tutawapiga faini na kuwachukulia hatua kali za
sheria, mwisho tunaombeni sana tutii sheria bila shuruti, suala la kupigana faini sio jambo zuri sana , lakini na
nyie wananchi mtoe ushirikiano kwa Viongozi wenu unapomuona mtu anatupa taka
hovyo mpige picha au toa taarifa
tutamshurikia na kama kuna maeneo ni machafu
toa taarifa kwa Viongozi wenu tuyafanyie kazi tuanataka mji wetu uwe
msafi na kuwa Halmashauri ya mfano hapa nchini Amesema Kipako.
Mwisho, amewaomba Watendaji wa Kata kufuatilia
kwa umakini fomu za usafi zinazojazwa na Maafisa afya kabla haizjafika makao
makuu ya Idara,lakini niombe ushirikiano huu tuufanye sisi Kata, Mitaa pamoja na Maafisa wa Afya ili zoezi la Kampeni.
Post a Comment