MANISPAA YA MOROGORO YAPONGEZWA KUPATA HATI SAFI YA UKAGUZI HESABU ZA SERIKALI KIPINDI CHA MIAKA 4 MFULULIZO KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019.
RC Morogoro Loata Sanare akiongoza Kikao cha Baraza Maalum Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mei 22 mwaka huu 2020. |
Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo (kushoto) akiteta jambo katika kikao hicho na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo.
Baadhi ya Wahe. Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wakiwa katika kikao cha Baraza hilo Maalum. |
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare, ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za Seriklai kwa miaka 4 mfululizo wa mwaka wa fedha 2018/2019 huku akitoa rai kwa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na watendaji wake kuendelea kulinda mafanikio waliyofikia ya kupata hati inayoridhisha kwa muda wa miaka minne mfululizo.
Rai hiyo imetolewa Mei 22 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kujadili taarifa na majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
“Aidha ni wajibu wa Baraza sasa na menejimenti hii na Halmashauri kwa ujumla, kuyalinda mafanikio ya miaka yote hiyo ili msije angukia pabaya katika ukaguzi unaoendelea tena mwaka huu”. Alisema Sanare
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ametumia fursa hiyo kuwapongeza Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kufanikiwa kukusanya mapato ya ndani mwaka 2019/2020 zaidi ya asilimia 80 na kukidhi vigezo vilivyotolewa na TAMISEMI, vya kukusanya mapato hayo kwa asilimia 100 au zaidi ya asilimia 80 na si chini ya hapo.
Akiongea wakati wa kikao hicho, Loata Sanare amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata zao ili wananchi ambao ndio walipakodi wafaidi matunda ya kodi zao.
Naye Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga amesema Halmashauri hiyo imekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na mafanikiio katika ukusanyaji wa mapato yake ya ndani.
Amebainisha kuwa Makisio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ilikuwa shilingi 5,657,774,428.00, mapato halisi yaliyokusanywa ni shilingi 5,270,626,176.00. Wakati mwaka wa fedha 2019/2020 makisio ya mapato yalikuwa shilingi 6,705,926,212.87 na mapato halisi yaliyokusanywa ni shilingi 5,642,459,647.45 sawa na asilimia 84.14
Amesema mafanikio hayo yote yametokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya serikali, madiwani na chama Tawala na kuomba ushirikiano huo uendelee ili kuiletea maendeleo Halmashauri hiyo.
Rai hiyo imetolewa Mei 22 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kujadili taarifa na majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
“Aidha ni wajibu wa Baraza sasa na menejimenti hii na Halmashauri kwa ujumla, kuyalinda mafanikio ya miaka yote hiyo ili msije angukia pabaya katika ukaguzi unaoendelea tena mwaka huu”. Aalisema Sanare
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ametumia fursa hiyo kuwapongeza Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kufanikiwa kukusanya mapato ya ndani mwaka 2019/2020 zaidi ya asilimia 80 na kukidhi vigezo vilivyotolewa na TAMISEMI, vya kukusanya mapato hayo kwa asilimia 100 au zaidi ya asilimia 80 na si chini ya hapo.
Akiongea wakati wa kikao hicho, Loata Sanare amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata zao ili wananchi ambao ndio walipakodi wafaidi matunda ya kodi zao.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Eng. Emmanuel Kalobelo kupitia kikao hicho amezitaka Halmashauri zote Mkoni humo kuzitumia kwa wakati fedha zilizotengwa kwenye bajeti ya mwaka husika na kuepuka tabia ya kuchelewa kutumia fedha za baadhi ya miradi ya maendeleo hadi fedha hizo kumezwa na mfumo au kurudishwa Hazina, jambo ambalo ametaka lisifanyike kwa halmashauri yoyote.
Naye Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga amesema Halmashauri hiyo imekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na mafanikiio katika ukusanyaji wa mapato yake ya ndani.
Amebainisha kuwa Makisio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ilikuwa shilingi 5,657,774,428.00, mapato halisi yaliyokusanywa ni shilingi 5,270,626,176.00. Wakati mwaka wa fedha 2019/2020 makisio ya mapato yalikuwa shilingi 6,705,926,212.87 na mapato halisi yaliyokusanywa ni shilingi 5,642,459,647.45 sawa na asilimia 84.14
Amesema mafanikio hayo yote yametokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya serikali, madiwani na chama Tawala na kuomba ushirikiano huo uendelee ili kuiletea maendeleo Halmashauri hiyo.
Kihanga alisema kuwa , pamoja na mafanikio hayo kuna changamoto zilizojitokeza katika ukusanyaji wa mapato ambapo wafanyabiashara katika halmashauri hiyo wamekuwa wakikwepa kulipa kodi halali kwa kutoa visingizio mbalimbali, lakini bado halmashauri inaendelea na jitihada za kutoa Elimu kwao kujua umuhim wa kulipa kodi.
Naye Mkurugenzi Manispaa Morogoro Sheilla Lukuba, ameipongeza Menejimenti ya Manispaa ya Morogoro pamoja na Watumishi wote wa Idara ya fedha na Biashara kwa kuweza kutoa ushirikiano na kutumia utaalamu wao katika kuandaa taarifa ya Hesabu za mwisho na kujibu hoja kwa kujituma wakati wote was utekelezaji wa kazi hiyo.
" Haya ni mafanikio makubwa sana kwetu, kwani kitendo cha kupata hati ya ukaguzi inayoridhisha kwa muda wa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2015/2016 imetokana na utendaji kazi mzuri tunaouonesha" Alisema Lukuba.

Mwisho, alichukua nfasi ya kutoa shukrani zake za dhati kwa Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Madiwani ya Manispaa Morogoro kwa ushirikiano wa dhati waliouonesha katika kipindi Cha uwasilishwaji hoja za ukaguzi.
Baadhi ya Wahe. Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wakiwa katika kikao cha Baraza hilo Maalum
Post a Comment