Mkurugenzi Manispaa awaonya Wakandarasi wazawa kuacha tabia ya kujikongoja wanapoaminiwa kupewa miradi mikubwa.
Eneo la Ukumbi linavyoonekana kwa juu. |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ujenzi wa kitega Uchumi DDC.
Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng. Juma Gwisu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye mradi wa ujenzi wa DDC.
Ziara ya kukagua mradi wa Stendi mpya ya Daladala Mafiga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng. Juma Gwisu pamoja na wakandarasi wa ujenzi wa Stendi mpya ya daladala mafiga wakiwa wamekaa katika moja ya vituo vya abiria.
Muonekano wa Vituo vya abiria kwa ajili ya kusubiria usafiri vikiwa vimemalizika .
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,
amewaonya Wakandarasi wazawa kuacha tabia ya kujikongoja wanapoaminiwa na
kupewa miradi mikubwa katika Manispaa yake , huku akionyesha kutoridhishwa na kasi ndogo ya Ujenzi wa Kitega Uchumi DDC unaoendelea kwa
sasa.
Hayo ameyasema leo Mei 13,2020 wakati wa ziara yake ya kukagua miradi
ya maendeleo inayoendelea Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Lukuba ,amesema kuwa ni
lazima wahakikishe miradi wanayokabidhiwa na Serikali inakamilika kwa wakati.
Kufuatia kudolora kwa ujenzi wa DDC, Lukuba,
amemuagiza Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng.Juma Gwisu, kuhakikisha muda
waliopewa wa ujenzi wa mradi huo wakamilishe na hana mpango wa kuongeza muda
mwengine.
“”Hawa ndugu zetu tuliwaamini sana , walianza kwa
kasi kubwa licha ya kuwaongezea muda lakini bado sijaridhishwa na kiwango cha
Ujenzi wa mradi huu,nimeongea na msimamizi wa mradi huu analeta sababu zisizo na msingi wakati tayari tumelipa fedha, najua waliomba waongezewe muda lakini hapana ni bora ningekuta kuna
maendeleo ninge fikiria lakini bado hali ipo vile vile “ Amesema Lukuba.
Aidha, amemtaka msimamizi wa ujenzi huo kuongeza
nguvu kazi ili ujenzi uendelee kwa kasi kwani muda uliobakia ni mdogo sana.
Lukuba, amesema kuwa, kwa mujibu wa mkataba ujenzi huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 635, ulitakiwa kukabidhiwa mwezi Mei 20,2020 lakini mpaka sasa haujakamilika licha ya kuongezewa muda wa mwezi 1 ambapo sasa watatakiwa kuukabidhi mwezi Mei 25, 2020.
Katika hatua nyengine, Lukuba, ameridhishwa na kasi
ya ujenzi wa Stendi mpya ya Daladala Mafiga huku akimtaka Mkandarasi wa mradi
huo kuongeza kasi zaidi na kuukabidhi
mradi huo kwa wakati kama walivyokubaliana.
“Nimefurahishwa na kasi ya ujenzi huu wa Stendi ya
daladala , tumekubaliana mpaka ikifika Mei 25,2020 wawe wametukabidhi mradi
huu , niwaombe waongeze kasi ili tukabidhi mradi huu kwa wananchi ambao
wamekuwa wakiusubiria kwa hamu sana, endeleeni kufanya kazi usiku na mchana
natumaini hiyo asilimia 4% iliyobakia mtaimaliza kwa wakati”” Amesema Lukuba.
Hata hivyo, amewaeleza wananchi wa Manispaa ya
Morogoro kuwa Serikali yao ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ipo makini na itahakikisha ina kamilisha kwa
asilimia 100 miradi yote ya maendeleo ili kuendelea kutoa huduma bora kwa
wananchi.
Mwisho, amewataka wakandarasi wote wanaosimamia
miradi katika Manispaa ya Morogoro, wafanye kazi kulingana na walivyosainiana mikataba
kwani fedha ambazo wanatumia ifikapo mwezi
Juni 30, 2020 zitarudishwa hivyo kuna athari ya wenye miradi na
waliochukua tenda kuzikosa fedha hizo.
Kwa upande wa Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng.
Juma Gwisu, amesema atahakikisha fedha za miradi hazirudi Serikalini , hivyo
atakula nao sahani moja wakandarasi ili
fedha hizo ziendelee kutumika katika miradi hiyo.
Gwisu , amesema ujenzi wa mradi wa Stendi ya
Daladala Mafiga mpaka sasa umefikia asilimia 96% huku miradi mingine ikiendelea
vizuri na ujenzi.
Post a Comment