Mkurugenzi Manispaa Morogoro atimiza ahadi yake ya kukabidhi Sukari na Mchele Makao ya kulelea yatima Dar Ul Muslimeen.
Watoto wakimuombea Dua Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, mara baada ya kupokea vyakula hivyo kwa ajili ya Sikukuu ya Eid Fitir. |
MKURUGENZI wa Manispaa ya
Morogoro, Sheilla Lukuba, ametimiza ahadi yake ya kukabidhi Sukari kilo 50 pamoja na Mchele kilo 50 katika Makao ya kulelea Watoto yatima ya Dar
Ul Muslimeen yaliyopo Kata ya Mbuyuni.
Msaada huo wa Sukari na
Mchele umekabidhiwa leo Mei 20,2020
kwenye Makao hayo na Afisa Ustawi wa
Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa.
Akizungumza na Waandishi
wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi, Sidina, amesema kuwa lengo na chakula hiki
ni moyo wa Mkurugenzi kutaka kula Sikukuu hii na watoto kwani nyuma
alishatangulia kutoa vyakula kwa ajili
ya mfungo nahii ni awamu ya pili kama sadaka yake.
“ Mkurugenzi wetu
anawapenda amenituma nilete salamu hizi na amesema anawapenda sana watoto
angetamani afanye zaidi lakini kwa hiki kidogo ameona akitoe ili kuungana na
nyinyi katika Sikukuu hii kubwa , amepokea
barua yenu ya shukrani na ameshukuru sana kwa kutambua mchango wake, nafikiri
mwanzo tulishaleta vyakula na akaahidi
kwamba ataleta sukari na sasa sukari
imekuja , hakuishia hapo ameona ni vyema akaungana na nyie katika kusherekea s
Sikuu ya Eid Fitir kwa kuwaletea Mchele kiasi cha kilo 50 na Sukari kilo 50
ambapo awali aliahidi kilo 25 lakini akasema hapana lazima aongeze na kufikia
kilo 50 ambazo leo tunawakabidhi, kikubwa mzidishe maombi kwake, kwa Viongozi
wengine ikiwemo Mkuu wa Wilaya , Mkuu wa Mkoa na Mhe. Rais Dkt John Magufuli
ili wazidi kulitumikia Taifa wakiwa na
afya tele”Amesema Sidina.
Aidha , amewataka Watoto
kuongeza juhudi katika masomo ili waweze kufikia ndoto zao , na sula la
kuondokewa na wazazi lisiwafanye warudi nyuma.
Kwa upande wa Matroni wa Makao
hayo, memshuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa kuwa
karibu sana na Wananchi wake jambo ambalo linatia matumaini.
“’Tunampongeza sana
huyu mama , kwanza ni mchapakazi lakini sio msaada wa kwanza kutupatia
alishawahi kutukabidhi ndoo za maji , beseni na sabauni kwa ajili ya kujikinga
na CORONA hii imeonesha ni jinsi gani amekuwa karibu na wananchi wake hatuan
cha kumlipa kikubwa tunamuombea dua Mwenyezi Mungu alinde na kumbariki na
kumuongezea zaidi ya kile alichokitoa, hatuishii kwa shukrani tu bali
tutamuandikia barua rasmi ya kumshukuru kwa msaada wake wa kutusadia katika
kupata futari kwa watoto wetu “ Amesema Khadija.
Pia alienda mbali
zaidi kwa kuwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu Viongozi wote
wa Mkoa wa Morogoro akiwemo Mkuu wa Mkoa, Mhe. Loata Sanare, Mkuu wa Wilaya
Mhe. Regina Chonjo, Mkurugenzi wa Manispaa , Sheilla Lukuba na
Viongozi wengine kwa kushirikiana vyema katika kupambana na janga la Ugonjwa wa
CORONA .
Post a Comment