DC CHONJO APOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA KUTOKA KAMPUNI YA TAZAMA PIPELINE LIMITED VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 4,800,000/=
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amepokea
vifaa vya kunawia mikono vyenye thamani ya Shilingi 4,800,000/= vikiwamo stendi
za kuwekea ndoo za kunawia mikono 8, mashine ya kupima joto 5 , Barakoa pamoja na Vitakasa mikono pamoja na sabuni kutoka Kampuni ya Tanzania na Zambia ya kusafirisha mafuta
kutoka Tanzania kwenda Zambia (TAZAMA
Pipeline Limited kwa lengo la
kuwasaidia wananchi kujikinga na maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa
na Virusi vya COVID 19 (Corona).
Tukio hilo la kukabidhi vifaa tiba kutoka TAZAMA Pipeline
Limited limefanyika leo Mei 29, 2020 nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Morogoro.
Vifaa hivyo vya kujikinga
na maambukizi ya Virusi vya Corona vimepokelewa na Mkuu wa Wilaa hiyo Mhe. Regina
Chonjo,akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,
, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro Dr Ikaji Rashid e pamoja na Katibu Tawala
Bi Ruth John.
Akizungumza wakati
wakupokea vifaa hivyo, Mhe. Chonjo, amesema kuwa Wilaya ya Morogoro imepokea vifaa hivyo na kwamba wataendelea
kuhamasisha wadau wengine waweze kuchangia ili kuendelea kudhibiti ugonjwa huo
usisambae kwenye maeneo mengine.
Chonjo, amefafanua kuwa Virusi vya Corona vimekuwa janga
kubwa Duniani na kwamba Wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa kila mmoja
anatumia vitakasa hivyo ili kujikinga na maambukizi ya Virusi hivyo pasipo
kuambukiza wengine.
“Kama mkuu wa Wilaya
ninashukuru kwa msaada huu, kwetu, tutakuwa huru kwa kuendelea kutoa huduma kwa
wananchi kama kawaida, ndio mana mmeona hapa kila anaeingia ana nawamikono yake
kabla ya kuingia kupatiwa huduma” amesema Mhe. Chonjo.
”
kwetu sisi hatupambani kama Morogoro , tunapambana kama mkoa ,nandio jukumu
tulilopewa , hivyo hivyo nitumie fursa hii kuwaalika wadau wengine wenye
mapenzi mema kutupatia vifaa vingine” Ameongeza DC Chonjo.
Aidha,
ameeleza kuwa Wilaya hiyo imejipanga vizuri katika kupambana na virusi vya
Corona ikiwemo kuendelea kutoa matangazo ya kuhamasisha na kuelimisha wananchi
namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.
Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe.
Pascal Kihanga, amesema kuwa kutokana na suala la korona kuhusisha maisha ya
watu ni vema kila mmoja akautambua vizuri ugonjwa wa korona na kutoa elimu ya
tahadhari katika familia, nyumba za ibada kama vile makanisani na misikitini
huku akiendelea kusistiza kuwa suala la taarifa mbalimbali pamoja na matamko
dhidi ya korona yatakuwa yakitolewa na viongozi ili kutoleta taharuki katika ya
jamii.
“Niombe Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro na timu yake ya Wataalamu , hivi vifaa ni vya kisasa ukilinganisha na
tulivyokuwa tukivipata siku za nyuma, hivyo elimu inahitajika mahali popote
vitakavyowekwa ili visije kutumika vibaya , tumeona utumiaji ni rahisi sana
lakini lazima watu tuwaelekeze na ninaamini watu ni waelewa wakielekezwa
watavitumia vizuri” Amesema Mhe. Kihanga.
Akisisitiza tahadhari dhidi ya korona Mkurugenzi wa Manispaa
ya Morogoro, Sheilla Lukuba amesema kwa kuwa kuambukizwa kwa virusi vya korona
ni mawasiliano ya mtu na mtu kwa kubebaba virusi hivyo jambo kubwa na la
msingi ni kila mmoja kujitenga kwa maana ya kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya
lazima jambo litakalosaidia kuepusha maambukizi ya gonjwa hili ambapo amesema
kinga ni bora kuliko tiba na kwamba gonjwa la korona halina tiba hivyo ni vema
kuepuka maeneo ambayo ni hatarishi kwani litasaidia kuwa salama na kuepuka
maambukizi.
Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr Ikaji Rashid, amesema
njia ya kujikinga na ugonjwa huo ni kwa njia ya kuosha mikono vizuri kwa maji safi na
sabuni, kutumia vikinga pua na mdomo (masks)na uso, kuzingatia walau umbali wa
futi 6 kutoka kwa mgonjwa mwenye korona, Hakuna chanjo mpaka sasa ambapo
amesema kirusi cha korona katika mwili wa binadamu huchukua siku 2 mpaka
14(wastani siku 5) kwa binadamu kuanza kuonesha dalili baada ya kuambukizwa na
virusi vya koron pia huambukizwa kwa njia ya matone yatokanayo kwa kukohoa au
kugusana moja kwa moj lakini pia kuepuka kusalimiana kwa mikono.
Kwaupande wake Afisa Utumishi wa Tanzania kwenda Zambia (TAZAMA
Pipeline Limited, Msemwa Deogratius,amesema wameamua kutoa
misaada hiyo katika taaisis za Serikali na Vituo vya afya kwa ajili ya kuunga
mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kupambana na Ugonjwa wa CORONA.
‘”Misaada hii tumeielekeza katika maeneo yote ambayo Bomba
letu liempita, tumeanzia Kigamboni, Tunduma na maeneo mengine, na vifaa hivi
tiba vitawasaidia wananchi ikiwa ni hatua ya kujikinga na virusi hivyo vya homa
ya mapafu inayosababishwa na Covid 19’’ Amesema
Msemwa.
Hata hivyo amesema zoezi hilo pia lilifanyika katika Nchi ya
Zambia ambapo walianzia Wilaya ya Kinondoni na watamalizia katika Wilaya ya
Tunduma.
Post a Comment