Afisa Mwandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini, awataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa kwa masaa yaliyobakia.
Afisa Mwandikishaji wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,akizungumza na mmoja wa wasimamizi wa Kituo cha kujiandikisha . |
Afisa Mwandikishaji wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akinawa mikono mara mara baada ya kuwasili kituoni. |
Afisa Mwandikishaji wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba. |
AFISA Mwandikishaji wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini na Mkurugenzi wa
Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba amewataka wananchi wa Manispaa ya Morogoro
kujitokeza kwa wingi kwenda kuhakiki taarifa zao katika Uboreshaji awamu ya
pili Daftari la wapiga kura ajili ya uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2020.
Lukuba, ametoa wito huo leo Mei 4, 2020 kwenye Kituo cha Nguzo Shule ya Msingi , wakati alipokuwa akihakiki taarifa zake pamoja na kuwahamasisha wananchi wa Jimbo
la Morogoro Mjini, na Kata zote 29 zilizopo Manispaa ya Morogoro kujitokeza kwa
Wingi kuhakiki taarifa zao kwani masaa yaliyobakia ni machache.
Amesema kuwa maendeleo ya
nchi yanaanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata, wilaya hadi Taifa hivyo tiketi
ya kuweza kuchagua kiongozi mwenye sifa nilazima mtu awe amejiandikisha na
kuhakiki taarifa zake kama zipo sahihi ili aweze kwenda kumchagua kiongozi anayefaa.
” Tuna masaa machache sana , zoezi hili litamalizika saa 12.00 Jioni, Bila ya kujiandikisha wala kuhakiki taarifa katika Daftari la
Uboreshaji kamwe haitawezekana kumchagua
kiongozi mnaye mtaka hivyo wito wangu kwenu kwa haya masaa yaliyobakia kwa
ajili ya kuhakiki taarifa, kubadili taariifa na kujiandikisha jitokezeni kwa wingi vinginevyo
mtapoteza haki yenu ya kumchagua kiongozi mnaye mtaka” amesema Lukuba.
Amewataka wananchi hao kujitokeza
kujiandikisha bila kujali itikadi ya vyama vyao kwani maendeleo hayana
chama yapo kwa ajili ya watu wote.
Aidha,
amesema Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ni sehemu
muhimu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2020.
Mwisho, amesema Uboreshaji wa daftari hilo unahusisha, uandikishaji wapiga kura wapya ambao wametimiza umri wa
miaka 18 na wengine ambao watafikisha umri huo mwezi Oktoba, watu ambao
wamehamia maeneo mengine ya makazi na walipenda kuamishia taarifa zao huko,
wapiga kura ambao vitambulisho vyao vimeharibika au kupotea kupata vitambulisho
vipya pamoja na kuwaondoa kutoka kwenye
daftari la kudumu la wapiga kura watu waliopoteza sifa za kuwa wapiga kura,
kama watu waliofariki n.k.
Licha ya zoezi hilo , lakini amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kufuata ushauri wa Wataalamu wa Afya pamoja na Viongozi wa Kitaifa katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa CORONA.
"Vituo vyetu vyote tumeweka wasimamizi wa kuangalia utaratibu wa kuepusha msongamano wakati wa kuhakiki taarifa, halikadharika kuna ndoo za kunawia mikono pamoja na sabuni, hivyo jitokezeni kwa wingi wala msiogope zoezi hili wala halichukui muda mrefu na ukishamaliza kuhakiki taarifa zako rudi nyumbani au endelea na shughuli zako" Amesisitizia Lukuba.
Post a Comment