DC Chonjo akabidhi Chakula na fedha shilingi 200,000/= kwa ajili ya Watoto wanaolelewa na Msikiti wa Kingo kuelekea sikukuu ya Eid.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, akimunesha Katibu wa Msikiti wa Kingo, Ostadhi Suleimani Kassim Lukanda (kushoto) vyakula vyengine vilivyomo ndani ya gari ikiwemo Viazi mviringo gunia moja .
Kindoo cha mafuta na Gunia la Viazi. |
MKUU wa Wilaya ya
Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amekabidhi chakula na fedha taslimu kiasi cha
Shilingi laki 2 kwa Uongozi wa Msikiti wa Kingo kwa ajili ya Watoto wanaolelewa
na Msikiti huo kuelekea sikukuu ya Eid.
Chakula hicho na fedha
amekabidhi kwa Katibu wa Msikiti wa Kingo leo Mei 20 , 2020 Ofisini kwake.
Akizungumza na Waandishi
wa habari, amesema lengo la kutoa chakula hicho na fedha ni kujenga ukaribu na
watoto hao ili waendelee kujisikia kwamba Viongozi hawajawasahaulika na kujiona ni
sehemu ya jamii.
“Nimeona niwakumbuke
Watoto , naamini unapokuwa yatima kuna unyonge Fulani unakuwa nao kwenye jamii,
na katika kipindi kama hiki ni vigumu kupata mahitaji ambayo watoto wenye
wazazi wao wanayapata, naamini kwamba hakuna ubaguzi ama unyanyasaji ambao
mnawafanyia , lakini endeleeni kuwalea katika maadili na kuwapa elimu na kuwapa
mahitaji yao ya kawaida kama chakula, nguo na vyenginevyo ” Amesema DC Chonjo.
“”Nimetoa na fedha pia
nikiamini kwamba vyakula haviwezi kuliwa bila mboga, na sikukuu ndio watoto
wanatakiwa wale pilau , na wajisikie vizuri na kuona wanafanana na wenzao “
Ameongeza DC Chonjo.
Aidha, ameupongeza Uongozi
wa Msikiti wa Kingo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwalea watoto yatima ya
kujiona na kujisikia kwamba wapo katika jamii na wana wazazi wanao wajali.
Naye Katibu wa Msikiti wa
Kingo ambao ni msikiti wa BWAKATA Wilaya ya Morogoro Mjini, Ostadhi Suleimani
Kassim Lukanda, amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa moyo wa kujitolea na kuwaona
yatima ni sehemu ya jamii ambayo wanahitaji kupata malezi sawa na wengine.
Amesema alichokifanya Mkuu
wa Wilaya hawana cha kumlipa ila wanamuombea kwa Mwenyezi Mungu amlipe zaidi ya
kile alichokitoa na azidi kuwakumbuka na wengine kadri atakavyojaliwa.
Post a Comment