Waziri Jaffo asifia ubora wa Stendi ya Daladala Manispaa ya Morogoro.
Muonekano wa Stendi mpya ya kisasa Manispaa ya Morogoro. |
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mheshimiwa Seleman Jaffo(MB),(kulia) akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika ujenzi wa Stendi mpya ya kisasa ya Daladala Mafiga. |
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu . |
Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Juma Gwisu, (wapili kutoka kushoto) akitoa maelezo ya mradi wa Soko Kuu la Kisasa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mheshimiwa Seleman Jaffo(MB). |
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mheshimiwa Seleman Jaffo(MB).akitoa shukrani mara baada ya kupatiwa maelezo ya mradi wa Soko. |
Uezekaji wa Paa la Soko ukiendelea. |
Afisa Utumishi Manispaa ya Morogoro akikagua Vizimba vya Soko . |
Muonekano wa makabati ya kuhifadhia bidhaa katika Soko Kuu la Kisasa unavyoonekana. |
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mheshimiwa
Seleman Jaffo(MB), ameupongeza Uongozi wa Manispaa ya Morogoro kwa
usimamizi mzuri wa Stendi mpya ya
Daladala Mafiga Manispaa ya Morogoro kwani umekidhi viwango na ubora
unaotakiwa.
Hayo ameyasema Mei 31,
wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya Maendeleo inayofanywa Manispaa ya
Morogoro.
Akizungumza na Waandishi
wa habari, Waziri Jaffo, amesema amefurahishwa na Ujenzi huo na kumtaka
Mkandarasi wa ujenzi huo kukamilisha mradi huo kwa wakati ili wananchi waanze kuutumia
mradi huo.
“Mimi
sio mtu wa kusifia sifia lakini kwa hili naomba niseme,nyinyi Morogoro miaka 5
iliyopita hamkuwa na mambo kama haya ,
sasa hivi yote mmeyapata , lakini niseme stendi hii ni moja kati ya stendi bora kabisa
Tanzania. Ujenzi wake ni wa viwango, mimi binafsi nimeridhishwa sana na
ukamilishaji wa stendi hii, nawapongeza sana viongozi wote kwa usimamizi mzuri “”amesema
Waziri Jaffo.
‘’Siku ile nilivyokuja hapa nilipata kichefuchefu lazima
nizungumze ukweli,sikulizika na kazi nilivyokuja, Mkuu wa Mkoa naomba ni
kwambie katika Stendi ambazo nimeridhika nazo na hasa katika hii pichi ya
kupaki magari na Stendi zote
nilizotembelea hii stendi nimeridhika nayo, hata hii idadi ya vibanda vya kupumzikia
wasafiri mmewazidi wenzenu wa Kibaha ,Iringa na Singida, nah ii inawezekana ni
Manispaa ya Kwanza Tanzania yenye Kituo kikubwa cha Daladala “Ameongeza Waziri
Jaffo.
Jaffo, amesema
kilichobakia ni kuhakikisha wanamalizia Ujenzi wa Vibanda vya Mama lishe na wamamchinga kwa
Wajasiriamali katika kuleta manufaa kwa Wananchi wa Morogoro.
Pia amewataka Viongozi wa
Morogoro wamfikishie salamu Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz
Abood, kwa kuwa na bahati kubwa ya kuingiziwa miradi yenye tija katika Jimbo
lake.
Waziri Jaffo, amewataka Viongozi wa Manispaa ya Morogoro waendelee kumpa ushirikiano Mhe. Abood kwani amekuwa kiongozi mwenye kuwapigania wananchi wake akiwa Bungeni.
Amesema ,Abood ni miongoni
mwa Wabunge Matajiri Tanzania lakini bado amekuwa katika mstari wa mbele wa kuwapigania
wananchi wake kuhakikisha wanapata huduma bora.
Aidha , Waziri Jaffo
,amesema anafahamu kilio cha Wanamorogo cha kuwa na Hospitali ya Wilaya huku
jambo hilo akisema Serikali ni siku waiachie kazi hiyo wataifanya.
Aidha Waziri Jaffo
ameitaka Halmashauri kuendelea kuwa wabunifu, na kuisimamia kikamilifu stendi
hiyo ili kuongeza Mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kuwa nia na matokeo
ya mradi huo ni kuongeza Mapato kwa Halmashauri pamoja na kutoa huduma kwa wananchi.
Mwisho amewataka Viongozi
wa Manispaa ya Morogoro kusimamia mapato kwani tayari wana vyanzo vingi ambavyo
vitaifanya Manispaa hiyo kujitegemea na kuendeleza miradi mingine pamoja na
kuweka uongozi imara katika miradi yao ili kuleta tija ya malengo ya ujenzi wa miradi hiyo kama ilivykusudiwa .
Licha ya kuridhishwa na
hatua za mradi huo iliyofikiwa katika utekelezaji, lakini amewataka wale wote
wanaosimamia miradi hiyo ikiwemo na wa Soko Kuu la kisasa kuzidisha kasi ya ujenzi, na kuona mkandarasi anakuwa
Site masaa ishirini na nne kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na
kuzuia upotevu wa fedha za wanyonge zinazotekeleza mradi huo.
Akitoa taarifa ya ujenzi
wa stendi hiyo, Msimamizi wa Miradi
inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, Mhandisi James Mnene, kwa niaba ya Mkurugenzi amesema kuwa, Mradi huo Umetekelezwa kwa
gharama za Tshs Bilioni 4.4 bila VAT ambapo mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa Shilingi Bilioni 3.6 sawa
na asilimia 82 ya bajeti ambayo amaelipwa.
“Tunapenda kuishukuru sana Serikali ya Awamu
ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe
Magufuli, kwa kuipatia fedha Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya ujenzi wa Kituo
hiki,mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa Shilingi Bilioni 3.6 sawa na asilimia 82
ya bajeti amabyo wamelipwa kati ya Bilioni 4.4 ambazo ni gharama ya mradi bila
VAT , matarajio yetu wiki mbili zijazo tuwe tumeukabidhi mradi huu Manispaa na
wananchi waanze kuutumia mradi huu” Amesema Mnene.
Mnene, amesema mpaka sasa
Ujenzi wa Stendi hiyo umefikia asilimia 98,ambapo kazi zilizobakia ni kazi za
usafi pamoja na matengenezo ya vitu vidogovidogo kama vile utenegenezaji wa
Bustani kwa ajili ya kuweka manzari yaonekane vizuri.
Post a Comment