Header Ads

Rais Magufuli ahudhuria ibada ya askofu wa kikatoliki Mhashamu Isaack Amani

Rais Magufuli pamoja na Mhashamu Isaack AmaniHaki miliki ya pichaIKULU/TANZANIA
Image captionRais John Pombe Magufuli akimpongeza aliyesimikwa kuliongoza jimbo kuu la kikatoliki la Arusha
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wamehudhulia ibada rasmi kwa ajili ya aliyesimikwa kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Mtoto Yesu Jimbo Kuu Katoliki.
Aliyehutubia mahubiri ya leo askofu Yuda, alisisitizia juu ya ya mshikamano, akiongeza kuwa kanisa katoliki linahusika tu na mapatano kama Mungu alivyowaagiza.
Ibada ya leo ilikuwa ni fursa ya mapadri na masista( watawa) kupata baraka na kumkaribisha kwa kumshika mkono.
JanethHaki miliki ya pichaIKULU/TANZANIA
Image captionMke wa rais Magufuli , Mama Janeth Magufuli(kushoto) pia alipata fursa ya kumpongeza Mhashamu Isaack Amani
Rais Magufuli akiwasalimiaHaki miliki ya pichaIKULU/TANZANIA
Image captionRais John Magufuli pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasalimia mapadre wa kikatoliki waliohudhuria ibada ya kusimikwa kwa Mhashamu Isaack Amani kama askofu wa jimbo kuu la kikatoliki la Afrusha
Hatua ya rais Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kuhudhuria ibada hii ya kanisa katoliki nchini humo inaonekana kama ishara bora ya kurejesha uhusiano mwema na baadhi ya makanisa makuu ya kikristo likiwemo kanisa katoliki ambao wamekua wakiikosoa vikali serikali yake...Maaskofu waonya kuhusu Umoja na amani ya Tanzania
Rais John Pombe Magufuli aliwasalimia waumini wa kikatoliki JumapiliHaki miliki ya pichaIKULU/TANZANIA
Image captionRaisJohn Pombe Magufuli akiwapungia mkono waumini na viongozi wa kidini wakati wa ibada ya kusimikwa kwa Mhashamu Isaack Amani kama askofu wa jimbo kuu la kikatoliki la Arusha Jumapili
Licha ya kukosolewa, rais Magufuli alipuuzilia mbali mbali waraka wa maaskofu uliotolewa wakati wa kuanza kwa msimu wa Pasaka akisema hauna msingi wowote ule.Aliendelea kwa kusema pia kwamba mbona hakuna aliyetoa waraka wakati mauwaji ya Kibiti yakiendelea.
Rais Magufuli alisema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa rada za kiraia uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Majibu yake kwa waraka wa maaskofu aliyatoa wakati akiwapongeza wasaidizi wake, mawaziri, viongozi wa ulinzi na usalama pamoja na wasaidizi wengine, ambao amewasifu kwa kuendelea kutimiza majukumu yao...
"Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ndio maana tuko salama leo, ilifikia mahali hata kwenda Kibiti tu ni kazi. Hatukuona mtu yeyote analaani," alisema Dkt Magufuli...Magufuli akejeli waraka wa maaskofu Tanzania

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.