DC Mjema awataka Wahasibu kutoa taarifa sahihi kusaidia pato la Serikali
Na John Luhende
Mwambawahabari
Wanawake Wahasibu Tanzania, wametakiwa kuwa waaminifu na kutumia vyema utaalam wao katika kazi za uhasibu ili kuisaidia wanawake wengine ambao hawana taaluma hiyo katika matumizi ya fedha na Taifa ili kuweka uwazi wa matumizi ya fedha katika Taasisi za serikali na sekta binafsi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa chama cha Wahasibu wanawake TAWCA, ambapo amewashukuru wanawake hao kwa kuonyesha uaminifa na uchapakazi katika majukumu yao.
"Kwa kweli wanawake niwachapakazi na mmeonesha imani kubwa maana Nikiangalia katika kesi kubwa kubwa zinazohusisha ufisadi wanawake siyo wengi hii ni kuonyesha kuwa ninyi ni waaminifu" Amesema Mjema.
Ametaka kuendelea kujadiliana ili kutatua changamoto zao na kusema kuwa wanawake wanatakiwa kumuunga mkono Rais Magufuli katika kujenga Tanzania ya viwanda kwa kuweka mahesabu sawa katika maeneo yao ya kazi ili Tanzania iweze kuwa na Maendeleo kwa kiasi kikubwa.
Aidha DC Mjema kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu, Ameendesha harambee ya kuchangia chama hicho kipya ili kukuza mfuko utaokifanya chama hicho kujiendesha ambapo zaidi ya shilingi Millioni 11,zimechangwa na Wanachama.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAWCA, Bahati Geuze, amesema chama hicho kitawaapatia mafunzo wanachama wake kupitia chama cha Wahasibu Tanzania na yatatolewa na chama hicho na kuongeza kuwa chama hicho kimeanzishwa ili kuongeza hamasa kwa Wanawake vijana kupenda masomo ya fedha ambapo wameahidi kusaidia wanawake waliopo katika shule na vyuo ili kuongeza namba ya Wahasibu wanawake wenye sifa na Elimu.
Post a Comment