Header Ads

Je Zanzibar imekuwa ikitumia mbinu gani kuhakikisha uchumi wake unaimarika?

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Bi Amina Salum Ali
Image captionWaziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Bi Amina Salum Ali
Licha ya kisiwa cha Zanzibar kuwa na ardhi ndogo, huku pia ikiwa na mtaji na mapato midogo, imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha uchumi wake unaimarika.
Kwa mujibu wa Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Amina Salum Ali, uchumi wa Zanzibar sasa umekuwa kwa kwa asilimia 7.4 ingawa lengo kwa kipindi hiki ilikuwa kufikia asilimia 10, kuweza kufikia matarajio ya kuingia katika uchumi wakati, ifikapo mwaka 2020 na 2025.
Zanzibar imekuwa ikitegemea sana sekta ya utalii, Bahari na Kilimo katika kuimarisha uchumi wake.
Mojawapo ya sabuni ambazo malighafi zake zinapatikana visiwani Zanzibar na kutengenezewa huko
Image captionMojawapo ya sabuni ambazo malighafi zake zinapatikana visiwani Zanzibar na kutengenezewa huko
Akizungumza na BBC, Waziri Amina amesema wanaanza kuimarisha viwanda vya ndani kupitia sekta za kilimo, bahari na utalii kwa kuanza kufufua viwanda vilivyokufa kama vile vya chumvi.
Katika bajeti ya mwaka huu, Zanzibar imeanzisha wakala wa kushajihisha viwanda vidogo na vya kati, kutokana na kwamba Zanzibar ina wajasiriamali wadogo wengi.
Hali ambayo pia itaweza kuwajenga ili bidhaa zao ziwe na ubora na kukidhi viwango vya kimataifa.
Changamoto kubwa kwa wafanya biashara wa Zanzibar ni soko kwa bidhaa zao.
Sauti za Busara zilivyochangamsha Zanzibar
Changamoto nyingine hususan kwa wafanyabiashara vijana ni pamoja na kukosa masoko, mitaji, ya elimu ya kufanya biashara pamoja na usafirishaji.
Licha ya kwamba wafanyabiashara wengi wa Zanzibar wanategemea sana soko la Tanzania bara, lakini serikali imekuwa ikiwashauri kuzalisha pia bidhaa ambazo zitakuwa na soko la kimataifa.
Akizungumzia mahusiano ya biashara kati ya Zanzibar na Tanzania bara, Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Amina Salim Ali amesema jitihada zaidi bado zinahitajika.
Wanawake Zanzibar
Amekiri fursa nyingi bado hazijagunduliwa na ili kuwezesha hilo ni lazima kufanya kazi kwa ushirikiano, kwa wizara za pande zote.
Katika kuimarisha biashara na Tanzania bara, katika siku za hivi karibuni, Zanziba iliingia mkataba wa kununua chaki zinazotengenezwa katika mkoa wa Simiyu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.