Waziri Makamba awapa somo vijana na wasanii
Waziri wa Mazingira na Muungano, January Makamba ametoa ushauri kwa vijana maarufu na wasanii katika ukurasa wake wa Twitter.
Ushauri huu umechukuliwa na wengi wa watumiaji wa mitandao ya Twitter na Instagram kama muhimu kwa wasanii hasa baada ya kuibuka kwa matendo yasiyoakisi taswira njema kwa jamii kwa siku za karibuni.
Ujumbe huo umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza lakini tafsiri isiyo rasmi ni:
“Kwa wadogo zangu maarufu wa kike na wa kiume: umaarufu unabeba majukumu. Ushike kwa makini. Umaarufu unaweza kudumu kwa dakika 15 watu tukafurahi na kukuona muhimu – kisha maisha yakaendelea. Umaarufu pia unaweza kudumu milele, ukafa kimwili lakini jina lako lisife. Umaarufu pia unaweza kudumu na kufikia kiwango cha kukuharibu na kukuondoa kwenye mstari.”
Mmojawapo ya wasanii waliojibu ujumbe huo Twitter ni Vanessa Mdee ambaye ameshukuru.

Post a Comment