Header Ads

Sababu 6 Za Kukosa / Kuchelewa Kupata Hedhi

Kwa mwanamke kuchelewa kupata hedhi huwa hakushitui endapo mwanamke atakua anajua ni nini tatizo au sababu iliyopelekea yeye kukosa hedhi. Na majibu ya kuchelewa kwa hedhi hupatikana pindi hedhi hiyo inapochelewa.

Mfano kama ulikua unategemea kupata mimba, ikichelewa inakua ni dalili ya kwanza ya wewe kuanza kufikiria jambo ulilolitaka ninaelekea kutimia na hata ukatabasamu na kuwaza hatua nyingine ya kujipima nyumbani au kuenda hospitali. Na kama hukuwa umetarajia ndio hivyo tena mawazo ya kila aina yatakuja kichwa kutaka kujua kwanini hedhi yako imechelewa na pengine usipate majibu kabisa.

Hapa nimekuwekea sababu 6 zinazoweza kusababisha hedhi ya mwanamke kuchelewa, na nimefanya hivi kwa kutambua kwamba wanawake wengi hufikiria sababu moja tu endapo hedhi yao itakua imechelewa.

1 . Mimba
Hii ndio sababu ya kwanza kuja kichwani endapo siku za hedhi za mwanamke zitakua zimechelewa. Na inawezekana ukawa sahihi!! Na hii hutokea hata kama mwanamke alishapata dalili zote za kwamba siku zake za hedhi ziko njiani, ila siku uliyotarajiwa ishuke inakua haishuki. Mara nyingi huwa tunashindwa kabisa kujizuia kufikiria neno MIMBA!! Hata kama mtu anafahamu kabisa hakucheza rafu mwezi huo. Kwa ushauri tu ili usipatwe na msongo wa mawazo zaidi tafuta kipimo binafsi au kama ni ngumu pitia hospitali upate vipimo.

2 . Msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo huleta madhara katika mwili wa binadamu mara nyingi sana, mfano kuumwa kichwa, kuongezeka uzito, kuota vipele na hata vidonda vya tumbo, na kama nilivyosema awali , kama tayari umeshajua kwamba hedhi imechelewa msongo wa mawazo unaoupata kwa kufikiri sababu ni mimba ikiwa haukuwa umeitarajia unaweza kufanya mwili usiwe katika hali yake ya kawaida tena na hivyo kuendelea kusababisha kuchelewa kwa siku za hedhi zaidi na zaidi. Kwenye mwili wa mwanadamu kuna homoni mbili ziitwazo ‘adrenaline na cortisol’.

Hizi hufanya maamuzi kwenye mwili ya kipi kinaumuhimu zaidi ya kingine mpaka msongo wa mawazo utakapokuisha. Mara nyingi homini hizi huamua kuanza kazi katika vitu kama msukumo wa damu na gesi mapafuni, huku kazi nyingine kama mmeng’enyo wa chakula na mfumo wa kizazi kufuatia baadae  na hivyo hata hedhi itachelewa kushuka kama tatizo ndio hilo.

3 . Ugonjwa
Ugonjwa wowote unaweza sababisha hedhi kuchelewa kwa hedhi, hata kama ni mafua au malaria. Ugonjwa uliona kwa wakati huo utakua ni kipaumbele cha kila homini mwilini mwako kuundoa kama nilivyoelezea hapo juu kwa homoni zako kutoa kipaumbele kwa mifumo muhimu zaidi ya kizazi kwa wakati huo.

4 . Kubadilisha mazingira.
Kubadili mazingira kwa hapa naamaani chochote kile ulichokua unafanya zamani, ukakicha ghafla mfano ulikua unaishi sehemu ya baridi ukahamia yenye joto na kinyume chake, au kusafiri muda mrefu, kama ulikua unafanya kazi usiku tu ukaanza kufanya kazi mchana mara nyingi hii husababisha kukosa au kuchelewa kwa hedhi. Usihofu endapo unajua ulifanya nini mwezi huo.

5 . Kunyonyesha
Kama unanyonyesha hautaona hedhi kwa muda mrefu, japo hutofautiana kutokana na maumbile ya kila mwanamke kwa sababu prolactin ( Homoni inayowezesha uzalishaji wa maziwa ya mama ) huharibu kupevuka kwa yai (ovulation) . Wamama wengi hua hawapati hedhi kwa miezi pale wanapokua wananyonyesha . Lakini kumbuka , kukosa hedhi haimaanishi kwamba hauwezi kushika mimba , kwa sababu ovulation hutokea kabla haujapata hedhi yako, inawezekana yai likapevuka na baadae ukapata mimba kabla hata haujapata hedhi . Kwahiyo ukiwa unanyonyesha hakikisha unatumia kinga.

Madawa
Ukweli ni kwamba kuna dawa maarufu za kusababisha kuchelewa kupata hedhi. Hizi ni kwa matumizi ya uzazi wa mpango. Dawa hizi huzuia ovulation kwahiyo kama hakuna ovulation basi hakuna hedhi. Na hizi unaweza fahamu kama unazitumia kwa hiyo hedhi ikichelewa unakuwa huna wasiwasi, na kama hufahamu basi endapo utaongea na daktari anayekupangia dawa za uzazi wa mpango kumbuka kumuuliza madhara yanayotokana na matumizi ya dawa hizo (side effects) atakazokupa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.