Header Ads

Shina la CCM JPM Kariakoo lalaani maandamano ya kesho, yaita ni uhaini

SHINA la Chama Cha Mapinduzi CCM la JPM lililopo Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Jijini  Dar es Salaam limelani vikali kitendo cha watu watakaotaka kuandamana huku wakiita kitendo hicho uhaini na wanapaswa kuadhibiwa.
Image may contain: 3 people, people standing and shoes
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo kwenye Eneo la Shina hilo, Katibu wa Shina hilo, Ndugu Solomoni Anani Pemba, amesema hawakubaliani na hatua ya wahuni wachache wenye malengo ya kuharibu taswira ya nchi na amani ya Tanzania.



"Sisi kama Vijana wa Chama cha CCM , tunapinga vikali hatua hiyo, Rais wetu ndio kwanza anajenga nchi, iweje watu wachache wenye maslahi yao wanaotumiwana Mabepari watusumbue? watu kama hawa hawatufai katika nchi yetu tunahitaji kumpa muda Rais kwani mambo anayopigana nayo ni mazito yana mnyororo mkubwa hivyo kama wataendelea na msimamo wao basi tunaomba Jeshi mtumie kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Zamani, Mizengo Pinda ya Wapigwe tu"Amesema Anan 
Image may contain: one or more people
Naye upande wa Mwenyikiti wa Shina, Ndugu Hamisi amewataka Wananchi kuwa watulivu na wale wenye dhamira ya kutaka kufanya maandamano waache mara moja , huku akiwasihi Wanachama cha CCM wasiingie katika mkenge huo kwani kuingia kwao kunatia doa chafu katika chama.
Image may contain: 3 people, people standing and shoes

Image may contain: 3 people, people smiling, people standing and shoes
Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Shina hilo, Kaisi maarufu kwa jina la Dele, amewapongeza Jeshi la Tanzania kwa kuwa ngangari katika kujiandaa na watu wasiopenda maendeleo ya Taifa lao huku wakipiga debe Mataifa ya wenzao kama Vibaraka 
Image may contain: 1 person, standing

Hata Hivyo, Mjumbe Mwinyi maarufu kwa jiana la Batigo, amesema huu ni wakati wa kujenga Chama, hivyo nguvu zote waelekeze katika Chama ili kukamilisha ajenda ya Rais Magufuli ya Tanzania Mpya na CCM mpya.
Image may contain: shoes and text

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.