Wakuu wa Mikoa Tanzania na Kenya wakutana kujadili changamoto za mipaka na mazingira
Wakuu wa mikoa mitatu kutoka nchi ya Kenya na Tanzania wamewataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa mipaka ya nchi hizo kuwa wazalendo kwa kulinda na kutunza mipaka jambo ambalo litasaidia raia wa nchi husika kutambua mipaka ya nchi yake ikiwa ni pamoja na kuepuka migogoro ya mipaka inayoweza kusababisha maafa makubwa ikiwemo vita.
Hayo yamesemwa na wakuu wa mikoa kutoka katika nchi hizo katika ziara ya kuhakiki shughuli ya uimarishaji, uboreshaji na ujenzi wa bikoni mpya zinazotenganisha nchi hizo Mbili unaofanywa na wataalamu wa ardhi na mipaka kutoka kenya na Tanzania katika maeneo ya baadhi ya vijiji vinavyopakana na nchi ya kenya vilivyopo Katika mkoa wa Mara ambavyo ni kerongwe, kubitelele, kumwamu mtimuramu pamoja na silari huku jambo hilo likilenga kuwanufaisha wananchi wa kenya na Tanzania kwa kutambua mipaka ardhi pamoja na mashamba yao.
Adam malima ni mkuu wa mkoa wa Mara amesema kuwa mkoa wa Mara na serikali ya Tanzania kiujumla itakuwa tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali na wa dhati kwa wataalamu hao wa ardhi ili kuhakikisha ujenzi huo wa mpaka baina ya nchi hizo unatekelezwa kwa ufasaha
Pia mkuu wa mkoa wa Nyanza uliopo nchini kenya Moffat Kangi ameongeza kuwa kuwepo kwa uimara wa mpaka huo itasaidia kukua kwa umoja na ushirikiano pamoja biashara baina ya kenya na Tanzania
Kwa upande wake dokta James Mtamakaya ambaye ni Kaimu mkurugenzi wa idara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kutoka Tanzania amesema kuwa lengo la nchi hizo ni kujenga mipaka kilomita758 ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kujenga kilomita 25, nakuongeza kuwa kuanzia sasa wamejipanga ipasavyo na wataanza kujenga kilomita 4 kwa siku ambapo shughuli hiyo iliyoanza Mwezi wa tatu inatarajiwa kuchukua miezi mitatu na itakamilika 30 June mwaka huu

Post a Comment