Singida United, KMC mbioni kunasa saini ya mshambuliaji wa Yanga
Taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kuwa klabu za Singida United na KMC ya Kinondoni zinamnyatia winga wa Yanga, Geoffrey Mwashiuya.
Mwahiuya alijiunga na Yanga akitokea Kimondo FC na kuonekana kuwa mchezaji aliyeweza kupewa nafasi kubwa ndani ya kikosi hicho lakini kwa sasa amekuwa wa kuanzia benchi.
Taarifa zinaeleza tayari viongozi wa timu hizo mbili, KMC na Singida walishaanza mipango ya kimyakimya kutaka kumsajili Mwashiuya ili kuboresha safu za ushambuliaji.
Mchezaji huyo yuko na kikosi cha Yanga hivi sasa mjini Awassa, Ethiopia, akijiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha FC utakaopogwa Aprili 18 2018.
Post a Comment