Header Ads

Raia wa Syria wamuunga mkono rais Assad na kumshutumu Trump

Barabara za mjini Damascus zimejaa watu kama kawaida. Wanajeshi katika vizuizi wamepumzika huku vizuizi vya usalama vikipunguza operesheni zake kali.
Maduka yako wazi na watu wanaelekea kazini kama kawaida. Makumi ya raia wa Syria yamekongamana katika bustani kubwa mjini Damascus karibu na jengo la runinga ya Syria wakiunga mkono jeshi lao, Syria na rais Assad.
Wanasema kuwa wanataka kumwambia rais Trump kwamba hawamuogopi na kwamba hakuna kitakachobadilika kwa jeshi na kwa rais Assad.
Wengi walisema kuwa walitarajia shambulio hilo na kwamba hawadhani kwamba kutakuwa na shambulio jingine.

Urusi: Shambulio la Syria litaathiri mazungumzo ya amani



Shambulio la angani dhidi ya Syria litaathiri mazungumzo ya amani , msemaji wa Urusi amesema kulingana na chombo cha hanbari nchini humo RIA.
Maria Zakahrova alisema: Kitendo hiki kinatoa ishara kali kwa watu walio na itikadi kali na wapiganaji kwamba wanatekeleza vitendo vya sawa.

Raia wanaomuunga mkono rais Assad nchini Syria wakiandamana na kupinga mashambulizi dhidi ya Syria
afp
Raia wanaomuunga mkono rais Assad nchini Syria wakiandamana na kupinga mashambulizi dhidi ya Syria

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.