Rais wa Ufaransa afanya ziara nchini Marekani
Rais Macron katika ziara yake hiyo atazungumza na rais wa Marekani Donald Trump. Katika ziara yale hiyo masuala mauhimu ya ushirikiano baina ya Marekani na Ufaransa yatajadiliwa ikiwemo pia ushirikiano na Umoja wa Ulaya.
Rais Macron amefanya mahojiano katika kituo cha runinga cha Fox News katika mkesha wa safari yake kuelekea nchini Marekani. Macron akizungumzia kuhusu jeshi la Marekani kuondoka Syria, amesema kuwa ambo itakuwa kuicha ardhi ya Syria chini ya milki ya Iran na Bashar la Assad.
Jambo muhimu katika ziara hiyo ya Macron nchini Marekani ni kumkenaisha rais wa Marekani Donald Trump kutobadilika kuhusu mkataba wa nyuklia na Iran uliosainiwa mwaka 2015.
Post a Comment