Header Ads

Wasichana wa Chibok: Mateka wengi wamefariki anasema mwandishi

Aisha Oyebode. muanzilishi wa vuguvugu la Bring Back Our GirlsHaki miliki ya pichaAFP
Image caption112 kati ya wasichana 276 wa shule ya Chibok waliotekwa mnamo 2014 bado hawajulikani waliko
Mwandishi habari wa Nigeria ambaye amekuwa akiwasiliana na kundi la wanamgambo wa kiislamu Boko Haram amedai kuwa ni wasichana 15 kati ya 112 waliotekwa wa Chibok ndio walio hai.
Wasichana hao 276 wa shule alitekwa nyara na Boko Haram miaka minne iliopita. Wengi wao wameachiliwa tangu hapo.
Ahmad Salkida anasema alijadiliana kwa niaba ya serikali na wanamgambohao ili waachiliwe, lakini nafasi nyingi zilipotezwa kulifanikisha hilo.
Serikali ya Nigeria inasema hakuna sababu ya kufikiria kwamba baadhi wamefariki.
Msemaji mmoja ameiambia BBC kwamba serikali ingali inajadiliana na Boko Haram kufanikisha kuachiwa kwa wasichana hao 112 ambao bado hawajulikani waliko.
#BringBackOurGirls t-shirtsHaki miliki ya pichaAFP
Bwana Salkida amesema utawala wa rais wa zamani Goodluck Jonathan hulimuomba ajadiliane na kundi hilo ili wasichana wa shule ya Chibok waachiliwe wiki mbili baada ya kutekwa.
Alisema kwamba alifanya mipango ya kukabidhi wafungwa watakaoachiliwa wa kundi hilo mara tano , lakini kuchelewa kwa serikali iliyokuwepo wakatihuo ulichangia kuvunjika kwa majadiliano yaliokuwepo.
Salkida hakutaja majina ya wasichana waliosalia, akieleza kwamba hilo ni jukumu la serikali ya Nigeria.
Wazazi wa wasichana hao walifanya kumbukummbu ya mwaka wa nne Jumamosi tangu kutekwa kwa wasichana hao kwa kuandamana na maelfu ya watuwengine hadi katika shule hiyo kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno mahlai ambako wasichana hao walitekwa mnamo 2014.
Kwa wazazi wa wasichana ambao waliachiwa huru, walivaa nguo nyeupe katika kumbukumbu hiyo ya imani tofuati, shirika la habari la AFP linaripoti - na kwa wale ambao watoto wao bado hawajajulikana waliko walivaa nguo nyeusi.
"Ombi letu la kipekee ni kwamba wasichana wetu waachiwe na turudishiwe," Mzazi mmoja, Hannatu Daudu, salisema katika hadhara iliyokuwepo.
"Tunahitaji kujuwa iwapo wako hai au walifariki. Kama wako hai, basi nawarudi nyumbani , na kama wamekufa basi tujulisheni , ili angalau tuweze kuwaombea na tupoea uchungu tulio nao."

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.