Header Ads

Kumbilamoto amuomba RC Makonda kuongea na wamiliki wa Kampuni za Magodoro kushusha bei kwa Waathirika wa Mafuriko


DIWANI wa Kata ya Vingunguti ambae pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omar kumbilamoto, amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuzungumza na Wamiliki wa kampuni za Magodoro ili wadau watakao kwenda kununua Magodoro kwa ajili ya waathirika wa mafuriko wapate punguzo la bei.


Akizungumza jijini Dar es Salaam na wananchi wa mtaa wa Mji mpya mapema Leo hii, wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali vyenye thaman ya sh 4,349,000 kutoka katika Kampuni ya Lions club,amesema endapo  wadau hao wataweza kufanyiwa punguzo la bei katika kampuni za Viwanda itapelekea wahanga wengi kunufaika na msaada huo.

Aidha ameshkuru Makonda kwa kuweza kumletea wadau wa kutoa msaada kwa wanga wa mafuriko, huku akimtaka Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa,huku akiwasihi wale walio na chakula majumbani kwao kuwaachia wanyonge.

Kwa upande wake Mwakilishi wa kampuni hiyo,Mustansir Gulamhussein amesema kampuni yake imekua ikitoa misaada mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko lengo ni kuwasaidia katika kipindi ambacho shughuli zao zimesimama.

Amesema,wanaendelea kutoa msaada katika maeneo mengine ambapo dola 10 zimetengwa kwa ajili ya kununulia Magodoro na vyandarua, huku akiwataka wananchi hao kupokea msaada walioutoa kwani tatizo hilo limewaumiza watu wengi ambapo baadhi ya msaada  alioikbidhi ni Maharage kilo 500, Mchele kilo 105, Unga kilo 105, sabuni ya Unga roba psmoja chupa za chai pisi 24.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.