Mke wa mwana wa mfalme wa Uingereza amejifungua mtoto wa kiume

Mtoto huyo ambaye atakuwa kitukuu wa sita wa malkia, amezaliwa katika hospitali ya St.Mary iliyopo Lindo Wing huko mjini London .
Hali ya afya ya mama na mtoto inaendelea vizuri .

Ujio wa mtoto wa tatu wa mwana wa Mfalme na mke wake Catherine amezaliwa saa saa saba majira ya Afrika mashariki.

Familia zote wamepata taarifa ya ujio wa mtoto huyo na wanafuraha kwa habari hizo njema.
Mpaka sasa jina la mtoto mpya bado alijatangazwa.

Taarifa kutoka makazi ya malkia zinasema William alikuepo wakati mtoto huyo akizaliwa na majina anayoyapenda kwenye vitabu ni pamoja na Arthur, Albert, Frederick, James na Philip.

Salamu za pongezi zimetumwa kutoka kwa waziri mkuu wa nchi hiyo Bi.Theresia May na anawatakiwa furaha na maisha mema yajayo.
Post a Comment