TPDC yakabidhi mradi wa uunganishaji wa gesi asilia Ubungo
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi mradi wa uunganishaji wa gesi asilia kutoka katika bomba kubwa la gesi asilia linalomilikiwa na TPDC kwenda kwenye bomba dogo la usambazaji wa gesi asilia kutoka Ubungo hadi Mikocheni ambalo nalo linamilikiwa na TPDC ili kuongeza kiasi cha gesi asilia katika bomba hilo kwa lengo la kuwafikia watumiaji wengi zaidi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba akikabidhi jukumu la ujenzi wa mradi wa uunganishwaji wa gesi asilia kutoka kwenye bomba kubwa la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam katika eneo la Valvu namba 15 (Block Valve Station-BVS) ambapo ndipo bomba hilo litarajiwa kujengwa hadi eneo la Ubungo Maziwa litakapounganishwa na bomba dogo la usambazaji wa gesi asilia kuelekea Mikocheni Dar es Salaam.
“Leo ni siku kubwa sana kwetu kama Kampuni ya Mafuta ya Taifa tunapokabidhi rasmi jukumu la ujenzi wa miundombinu ya kutoa gesi asilia kutoka kwenye bomba letu kubwa kwenda kwenye bomba letu dogo la usambazaji wa gesi asilia kazi ambayo itafanywa na kampuni ya SINOMA ambayo faida yake kubwa ni kulipa uwezo wa kubeba na kusambaza gesi nyingi zaidi itakayoruhusu uunganishwaji zaidi wa gesi asilia kwa watumiaji wapya katika maeneo yote ambayo bomba hilo linapita yaani Ubungo, Sinza, Chuo Kikuu, Survey, Mwenge na Mikocheni” alifafanua Kaimu Mkurugenzi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba akieleza kwa kina Mradi Mpya wa Kuunganisha gesi asilia kutoka bomba kubwa hadi kwenye bomba dogo la Ubungo Mikocheni mradi ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miezi miwili
Amesema kuwa, pamoja na kuendelea kusambaza kwa watumiaji wa zamani ambao ni MM I, MM II, MM III, TanPack na Iron and Steel wateja wapya watakaonufaika ambao tayari wameshakubaliana ni Coca Cola kwanza Limited na BIDCO na nyumba 70 katika awamu ya kwanza na kwamba wanatarajia kuunganisha kwa viwanda zaidi vitakavyokuwa tayari kwa muda wowote.
“Utaratibu wa uunganishwaji ni wa kawaida sana kikubwa mteja tarajiwa anatakiwa kuwasilisha barua ya maombi ya gesi asilia kisha wataalam kufanya utafiti wa namna ya kumuunganishia mteja gesi hiyo na kwa upande wa watumiaji wa majumbani tunashauri pia nyumba kadhaa kuungana pamoja na kuleta barua kisha taratibu za kiutalamu za namna ya kuwafikishia gesi asilia zifanyike" amesema Musomba.
Kwa upande wake Meneja Mkuu Msaidizi wa SINOMA ndugu Lu Xiaoqiang ambao ndio Wakandarasi walioshinda zabuni ya ujenzi wa mra
Akizungumzia gharama za matumizi ya gesi asilia majumbani Mhandisi Musomba amefafanua kuwa, “Matumizi ya gesi asilia ni ya gharama nafuu kulinganisha na mkaa na gesi za mitungi-LPG ambapo kwa mtumiaji wa gesi za mitungi mfano wa Kilo 15 ambayo itatumika kwa mwezi mmoja kama akitumia gesi asilia atatumia hadi miezi miwili na hivyo kuokoa karibu nusu ya gharama ya matumizi ya nishati majumbani lakini pia gesi asilia ni nyepesi kuliko hewa na hivyo kuwa salama zaidi kwa matumizi hata pale inapovuja kwa kuwa hupotea hewani.”
Jukumu la kusambaza gesi asilia ni la msingi kwa maeneo ya uchumi imara wa viwanda na hivyo TPDC inaendelea kufanya tafiti za kitaalamu za usambazaji wa gesi asilia katika maeneo mengine ya nchi yakiwemo Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Tanga na Dodoma.
Post a Comment