Header Ads

Naibu Spika afunguka na kuwakumbusha Wanaume



Naibu Spika, Tulia Ackson amefunguka na kuwakumbusha wanaume kiujumla kwa njia ya utani, kuwa hakuna umuhimu wowote kwa wao kufuatilia kipimo cha DNA ili kuweza kuthibitisha mtoto ambaye anamlea ni wake au laa, kwa madai kitanda hakiwezi kuzaa haramu

Mhe. Tulia ametoa kauli hiyo ya kuwafikisha ujumbe kwa baadhi ya familia wanaokumbwa au kusumbuliwa na kadhia hiyo katika Mkutano wa 11 wa kikao cha Bunge cha tatu kinachoendelea kufanyika katika mkoa wa Dodoma wakati alipokuwa anafunga kipindi cha maswali na majibu kwa siku ya leo Alhamisi (Aprili 5, 2018).

"Nilidhani wanawake tunataka kuandamana humu ndani Bungeni, watu tuna watoto wengi humu lakini kiswahili cha kawaida kabisa kinasema 'kitanda hakizai haramu' sasa unaenda kumpima wa nini", amesema Ackson.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kumekuwa na upotoshaji mkubwa katika jamii hasa katika suala la watoto ambao wengi wao huamini kuwa wanalea watoto ambao sio wao jambo ambalo ni upotoshaji.

"Sio kweli kwamba watoto 6 kati ya wote tunaoishi nao majumbani kwetu siyo wa baba au wazazi husika. Takwimu hiyo ilikuwa inatokana na wale wazazi waliyokuwa wanaenda kupeleka vipimo vyao vya  vinasaba 'DNA' ili kutambua uhalali wa mzazi lakini haina maana kwa ujumla wetu Tanzania nzima watoto wengi hususani wakina baba kuwa sio wakwao hilo jambo sio la kweli", amesema Dkt. Faustine.

Kwa upande mwingine, Dkt. Faustine amesema lengo la yeye kuweka sawa jambo hilo ni kutaka
wabunge na wananchi wengine wanaume wasiweze kukimbia majukumu yao ya msingi katika malezi.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.