Madrid yaibipu Man United

Madrid wameonesha nia ya dhati ya kutaka kutumia kiasi kikubwa cha fedha ambapo wanamikakati ya kutaka kuwasili kiungo Paul Pogba, Mshambuliaji Antony Martial pamoja na kipa david de Gea.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wanataka kuboresha zaidi kikosi chao ambacho kinaweza kikaachana na mshambuliaji wake Gareth Bale ambaye hivi karibuni imeripotiwa kuwa anaweza akaachana na timu hiyo.
Mbali na uhitaji wa wachezaji hao kuelekea Madrid, Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho naye ana mpango wa kuwasajili Gareth Bale, Toni Kroos pamoja na Luca Modric.
Endapo Madrid itafanikiwa kufanya usajili huo itakuwa imepiga hat trick kwa kusajili wachezaji watatu kutoka timu moja.
Post a Comment