Dismas Ten amjibu Manara maneno makali
Na George Mganga
Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten, amemjibu Haji Manara juu ya kile alichokiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram akilikejeli tangazo la timu hiyo linalowataka mashabiki wa Yanga kujitokeza Uwanjani kesho.
Yanga waliweka tangazo linaloonesha picha za akina dada waliovaa jezi la rangi ya njano likieleza kuwataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze wakiwa wamevalia uzi wa njano kuisapoti ikicheza dhidi ya Welayta Dicha FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Baada ya Afisa Habari wa Simba, Manara kuliona tangazo hilo aliandika ujumbe kupitia Instagram akieleza kuwa akina dada hao ni wanene na hawana maumbile mazuri kutumika kwenye tangazo hilo huku akiwaita mitulinga.
Kufuatia Manara kuandika hivyo, Ten amemjibu Manara kwa kumweleza kuwa akina dada hao ndiyo waliomchangia wakati anaumwa macho na kumfanya apelekwe hospitalini kufanyiwa matibabu.
"Asante ndugu yangu kwa 'kunitag' Ila naomba nikukumbushe tu, akina dada hao unaowaita 'Mitulinga' Leo.! Ndiyo waliotoa hela (tena waliyoitafuta kwa jasho lao) kukuchangia ukapate matibabu nauliipokea, dunia iliona. Hakika tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo" aliandika Ten.
Post a Comment