Header Ads

RC MAKALLA AAGIZA MAENEO YA WRONG PARKING YABANDIKWE VIBAO.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam .Mhe. Amos Makalla,(kushoto) akizungumza wakati wa kikao .

- Aagiza waliojipa majukumu ya kunyemelea kukusanya Wrong Parking wasakwe Mara moja.

- Ataka TARURA na Wakurugenzi kutoa elimu na kuweka Vibao. 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam .Mhe. Amos Makalla, amezielekeza Halmashauri kwa kushirikiana na TARURA  kuhakikisha wanaweka vibao vya Wrong Parking  kwenye maeneo yasiyo rasmi kwa maegesho ili kuepuka uonevu.

RC Makalla, amesema hayo wakati wa kikao alichohitisha baina yake, Wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA  kilicholenga kuondoa kero ya tozo ya Wrong Parking.

Aidha RC Makalla, amesema kikao hicho wamekubaliana tozo ya Wrong Parking itekelezwe kwa mujibu wa Sheria lakini kwa mtu ambae ataonekana alidhamiria moja kwa moja kuvunja Sheria huku akisisitiza ,Elimu iendelee kutolewa.

Pamoja na hayo ,RC Makalla, ameamua kuunda timu ya wataalam kwajili ya kuandaa *mfumo mzuri wa Mapato ili kuhakikisha kiasi Cha tozo kinacholipwa kinaenda moja kwa moja serikalini na muhusika anapatiwa risiti ili kuepuka udanganyifu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.