MEYA MANISPAA YA MOROGORO AZINDUA MAGARI 2 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 110
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amezindua magari 2 yenye thamani ya shilingi milioni 110 yaliyonunuliwa na Manispaa ya Morogoro kupitia mapato ya ndani katika mwaka wa fedha 2020/2021 .
Tukio hilo la uzinduzi wa magari hayo limefanyika leo Julai 9/2021 nje ya Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Mhe. Kihanga, ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa ununuzi wa magari hayo ambayo yatasaidia sana katika kuongeza ukusanyaji wa mapato kwani Manispaa hiyo imekuwa na uhaba wa magari ambayo ymekuwa nguzo muhimu ya kusafirisha watumishi katika maeneo ya kazi hususani ukusanyaji wa fedha.
Kihanga, amewataka Watumsihi Manispaa ya Morogoro kuyalinda magari hayo na kuyafanyia huduma mara kwa mara ili yaendelee kutoa huduma.
" Mmefanya jambo zuri sana, tunaamini sasa tunakwenda kurahisisha kazi katika majukumu yetu, haya magari ni mapya kabisa yanahitaji sana huduma za mara kwa mara , msiyatumie mpaka mkayasusa na kuyatelekeza, gari ukilitelekeza sana linaongezeka ubovu, sasa sitarajii kuyaona yakiwa na hali mbaya maana mkifanya hivyo mtajikuta mmepoteza fedha zenu bure " Amesema Kihanga.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, amesema gari hizo zimenunuliwa kwa kiasi cha shilini 110,984,860 ambapo kwa gari moja limegharimu kiasi cha shilingi 55,492,430 kupitia kwa wakala wa huduma za ununuzi Serikalini, GPSA.
Waluse amesema mara baada ya GPSA kukamilisha mchakato wa manunuzi ikiwemo kuyakagua na kuyasajili waliwakabidhi kwa ajili ya kuendelea na kazi iliyokusudiwa.
"Taratibu zote zimefuatwa kikamilifu katika ununuzi wa magari ikiwemo kupta kibali kutoka kwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma ambapo kila gari inauwezo wa kubeba abiria 4 pamoja na dereva , tunaamni magari haya yatatusaidia sana katika shughuli zetu za maendeleo na tunaahidi kuyatunza na kuyafanyia hudma mara kwa mara " Amesema Waluse.
Manispaa ya Morogoro imenunua aina ya magari ya New Suzuki Jimny yenye namba za usajili wa SM 13779 na SM 13780 yenye ukubwa wa inji (Engine Cpacity ) ya 1462 .
Post a Comment