Header Ads

MAAFISA KILIMO NA UGANI MANISPAA YA MOROGORO WATAKIWA KUTOA TAKWIMU HALISI ZA KILIMO.

Afisa Kilimo Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo rejea ya ujazaji wa fomu za taarifa za mfumo wa Upatikanaji wa Takwimu na Taarifa wa Sekta ya Kilimo ARDS (Agricultural Routine Data System).

Washiriki Maafisa Kilimo.


Wakufunzi.

Washiriki Maafisa Kilimo.

MAAFISA Kilimo na Ugani Manispaa ya Morogoro wametakiwa kutoa takwimu sahihi za kilimo katika maeneo yao kwa kuzingatia mfumo wa upatikanaji wa taarifa wa ARDS (Agricultural Routine Data System).

Kauli hiyo imetolewa Julai 01/2021 na Afisa Kilimo Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, wakati wa uzinduzi wa mafunzo rejea ya ujazaji wa fomu za taarifa za mfumo wa Upatikanaji wa Takwimu na Taarifa wa Sekta ya Kilimo ARDS (Agricultural Routine Data System).

Akizungumza na Maafisa hao , Waluse, amesema mafunzo hayo wayatumie ipasavyo ili kuhakikisha kwamba yale mapungufu yaliyokuwa yanajitokeza katika taarifa zao yasiweze kujitokeza tena.

"Mafunzo haya yana umuhimu mkubwa , Manispaa yetu kwa kutambua umuhimu wake tumeweza kutenga fedha kupitia makusanyo ya ndani kwa ajili ya kuendeleza idara ya kilimo kwa kuwawezesha kutumia mfumo huu katika kukusanya taarifa na takwimu, niwaombe sana mafunzo haya yatumike kwa vitendo zaidi kwa sababu takwimu ni jambo la msingi sana " Amesema Waluse.

Aidha, amewataka Maafisa Kilimo hao kuhakikisha kwamba  vitabu vya fomu za kutoelea taarifa maalumu  ambavyo vimetengenezwa vitumike ili kuweza kujaza taarifa hizo.

Waluse, amesema kwa sasa Idara ya Kilimo ipo katika hatua za kusajili wakulima katika mfumo wa M-Kilimo na kuwata Maafisa Kilimo kuhakikisha kwamba takwimu wanazozitoa ziendane  na hali halisi ya kilimo katika maeneo yao ya Kata.

Hata hivyo,amesema baada ya mafunzo hayo matumaini yake ni kuona kunapatikana takwimu sahihi za wakulima katika Manispaa ya Morogoro.

Mbali na wakulima watakao wasajili , amewataka Maafisa ugani kuhakikisha wanapitia hekari  zinazolimwa na wakulima hao  ili wanapoenda kufanya maboresho ya kuwatambua wakulima basi wajue wakulima Manispaa wapo wangapi na wanalima eneo kiasi gani. 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.