Header Ads

WASHIRIKI MISS MOROGORO 2021 WATAKIWA KUTUMIA UREMBO KAMA NGUZO YA KUFIKIA NDOTO ZAO.

Miss Top Model Emmanuel Silayo (kushoto) akiwa na Miss Top Talent Chipegwa Julias (kulia) mara baada ya kuibuka washindi                  

                                                                                         
                                         
                
                                                              
                                                                      

WASHIRIKI wa  Shindano la kuwasaka warembo wa ulimbwende  Wilaya ya Morogoro maarufu kama Miss Morogoro  2021 wametakiwa  kuhakikisha wanatumia urembo wao kama nguzo ya kuzifikia ndoto zao.

Kauli hiyo imetolewa  Julai 23/2021 na mwakilishi wa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Rona Lyimo, aliyewahi kuwa Miss Morogoro mwaka 1995  akimwakilisha Mbunge huyo Mhe. Norah Mzeru katika uzinduzi wa Shindano la kumsaka Miss Morogoro 2021 lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Oasis Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo,Rona, amesema kuwa  Ulimbwende ni moja ya njia za kuonesha mchango katika jamii, lakini hilo litafanikiwa ikiwa walimbwende hao watajitambua na kusimama vema katika nafasi zao.

Hata hivyo, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan , kwa  kuonesha nia ya dhati katika kuendeleza tasnia ya sanaa ya Ulimbwende na urembo hapa nchini.

 “Ni lazima mtambue ya kwamba mna deni kubwa kwa Wilaya yenu na Kwa Taifa kwa ujumla la kutoa mchango chanya katika nyanja mbalimbali, rai yangu ni kwa washiriki wote kuwa tuzo hizi zisiende kuwa mapambo majumbani kwenu bali zikawakumbushe kuwa vipaji vyenu vinaweza kuwa ajira yenu , pamoja natambua kuwa kuna wasanii wa mziki, sanaa za maonesho , sanaa za mikono , ubunifu wa mavazi uwanamitindo na vipaji mbalimbali nawaomba muvitumie vipaji vyenu kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumbla lakini natambua kuna Vijana wanashindana katika katika kipengele cha miradi bora , basi miradi hiyo isibakie miradi ya kuwa kwenye makaratasi bali ifanywe miradi hiyo kwa maendeleo yenu na Taifa " Amesema Rona  

Rona, amesema  kuwa tangia awe mdau wa tasnia hii ya sanaa ya urembo ya ulimbwende haja wahi kusikia wala kuona skendo mbaya za washiriki jambo ambalo linaonesha ni kwa jisni gani Vijana wamejengeka kimaadili na kuwataka wale wanaoshiriki shindano la Miss Morogoro kulinda heshima zao na kuwa na maadili mazuri katika kuimarisha utamaduni wa Taifa.

"Hata nyinyi mtakao shinda msibweteke kwa kuwa washindi bali tuzo hizo zikawe chachu kwenu katika kufanya vizuri zaidi na kuongeza juhudi katika  kuviendeleza vipaji vyenu , hivyo nizidi kuwatia moyo tupo pamoja na tutazidi kuwa pamoja , Ofisi yangu ipo wazi muda na wakati wowote , njooni kwa ajili ya kujadili maendeleo mablimbali " Ameongeza Rona.

Mwisho, ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara nyengine zinazohusika na Vijana katika kuweka mfumo mzuri wa Vijana hao kuwatumia katika nyanja tofautitofauti ili kuongeza pato la Taifa huku akitoa mfano wa  Mkoa wa Morogoro  ambao una vyanzo vingi vya utalii ambapo Vijana hao wanaweza kutumika katika kutangaza vyanzo hivyo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mashindano ambaye ndiye muandaaji wa shindano hilo, Alexender Nikitas, amesema tuzo hizo zinafanyika katika vyuo mbalimbali Mkoa wa Morogoro zenye lengo la kugusa maisha ya Vijana walio katika vyuo wanaosoma taaluma na ufundi mbalimbali .

"Hizi ni tuzo zenye heshima kwa Vijana, tunawaomba sana washiriki mtambue kuwa vipaji vyenu mlivyonavyo ni zawadi ama karama mliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu , hivyo sisi kama wadau wakubwa wa sanaa ya ulimbwende tumeona ni vyema tukayapa uzito mkubwa sana mashindano yetu kwa kushirikiana na Serikali lakini Mama yetu Mhe. Mzeru amekuwa mstari wa mbele sana hata Miss Dododoma huyu mama amekuwa akisimama na mimi kuona mashindo kama haya yanafanikiwa " Amesema Nikitas.

Naye Katibu wa Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Ismail kifaru akizungumza kwa niaba ya Mhe. Norah Mzeru ,ameishukuru kamati iliyoandaa tuzo hizo chini ya Mkurugenzi wa mashindano Ndg. Alexender Nikitas na kuweza kumpa heshima Mhe. Norah  Mzeru, kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa Miss Morogoro 2021 ikiwa na  lengo la kuwasaidia Vijana kupitia tasnia ya sanaa ya urembo na ulimbwende.

Kifaru , amewashukuru washiriki wote wa shindano hilo, waandaaji wa shindano , wadhamini, wadau wakiwemo Manispaa ya Morogoro, Oasis Hotel, Pesps , Nikitas Miss Tanzania Morogoro,na Vyombo vya habari pamoja na wananchi wote waliohudhuria uzniduzi huo huku akiwaomba waendelee kuwa pamoja hadi fainali ya shindano hili litakapofanyika Julai 30/2021 katika Ukumbi wa Oasis Hotel.

Katika uzinduzi wa Miss Morogoro 2021, Chipegwa Julius aliibuka kidedea kwa kunyakua nafasi ya kuwa Miss top Talent na Emmanuela Silayo alifanikiwa kuchukua Miss Top Model.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.