Header Ads

MADIWANI MANISPAA YA MOROGOR0 WATAKIWA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO.

Mhe. Pascal Kihanga, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, akisoma Hotuba ya taarifa ya utekelezaji katika Mkutano wa mwaka wa  Baraza la Madiwani .

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Christine Ishengoma (kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse wakipitia taarifa za Mkutano wa mwaka wa Baraza la Madiwani.
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Christine Ishengoma akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma ,akipitia taarifa za Mkutano wa mwaka wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro.
Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia kwa ukaribu mkutano huo.

Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia kwa ukaribu mkutano huo.


Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia kwa ukaribu mkutano huo.
Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia kwa ukaribu mkutano huo.


MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka Madiwani waliochaguliwa mwaka 2020-2025 kuhakikisha wanabuni vyanzo vipya vya mapato tofauti na vyanzo vilivyobuniwa katika mwaka 2015/2020.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 9/2021 akisoma taarifa wakati wa kufungua Mkutano wa  Mwaka wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kihanga , amewataka madiwani kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vyanzo vilivyopo ili kuwezesha Manispaa  kuweza kuongeza uwezo wa kujitegemea kwa mapato ya ndani ya Manispaa. 

Kihanga, amesema kuwa awamu ya mwaka 2015-2020 kuna miradi mikubwa imefanyika , hivyo madiwani walioingia kipindi cha mwaka 2020-2025 wahakikishe kunapatikana vyanzo vipya na kuweza kuongeza mapato ya Manispaa.


Aidha, amesema kuwa Manispaa ikiboresha mapato itasaidia halmashauri kutoa huduma za jamii  kwa wananchi ikiwemo afya, elimu, Maji nk na  pia kiwango cha mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake itaongezeka.

"Mmeingia katika awamu hii ya 2020-2025, najua tumechanganyika wa zamani na wapya , hivyo tutumieni utaalamu wetu kuhakikisha tunabuni vyanzo vipya tofauti na mwaka 2015-2020, tunataka Manispaa tutoke hapa tulipo tufikie katika viwango vya Jiji, tumefanya makubwa sana miaka 5 iliyopita nategemea kwa Baraza hili tutavuka zaidi ya hapa tulipofanya" Amesema Mhe. Kihanga.

Katika hatua nyengine, Kihanga, amesema Manispaa ya Morogoro katika mwaka wa fedha 2021-2022 inategemea kukusanya jumla ya shilingi Bilioni 11,503,535,009.99 kupitia vyanzo vyake vya mapato .

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2021-2022  Manispaa ya Morogoro, imejikita katika vipaumbele vya ukusanyaji wa fedha, elimu, afya , Barabara , Usafi na Mazingira pamoja na Maji.

Amesema Manispaa katika mwaka wa fedha 2020-2021 imetekeleza miradi kama vile Soko Kuu la Chifu Kingalu Shilingi Bilioni 17, Kitega Uchumi DDC shilingi milioni 669, kufungua Soko la Nanenane kiasi cha shilingi milioni 69 ziliombwa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara, Kufungua huduma ya pamoja (One Stop Centre) kiasi cha shilingi milioni 37 , ujenzi wa madarasa Msingi na Sekondari milioni 280,000,000/= , maabara , matundu ya vyoo, ujenzi wa Zahanati milioni 229,000,000/= zimeshapelekwa.

Pia amesema Manispaa ya Morogoro inategemea kukamilisha miradi kama vile Gharama za awali za kitega uchumi DDC , kuanza kwa ujenzi wa kitega uchumi Soko la Manzese, kumalizia ujenzi wa Masoko 2, Kujenga Zahanati 1 kwenye maeneo ya pembezoni na upatikanaji wa huduma bora za afya, ujenzi wa shule mpya 3, ujenzi na umaliziaji wa miundombinu ya Elimu (vyumba vya madarasa 120, Ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi katika eneo la SGR , upanuzi wa kituo cha afya Sina, kumaliza Zahanati ya 5 zilizopo kwnye hatua mbalimbali, Ukarabati wa Ofisi ya Manispaa, kutoa mikopo ya asilimia 10 , kuandaa michoro 40 ya Mipango miji, kupima Viwanja 5000 vya matumiz mbalimbali, kuanza ujenzi wa machinjio ya Kisasa Manispaa kwa awamu 1 Kata ya Mkundi, kukarabati maeneo ya biashara Kitope 125, SIDO 46 na kumalizia ujenzi wa Vioski 16 vya Mafiga, kuendeleza Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa , kufunga mfumo wa umeme wa jua (Solar Power )  na CCTV Camera katika Soko la Chifu Kingalu pamoja na kuweka mifumo ya Maji Taka (MORUWASA) ya maeneo 3 ya umma ( Stendi ya Mafiga, Soko la Mawenzi na Soko la Mji Mpya).

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, amesema kuwa ukusanyaji  wa mapato ya ndani lazima uendane na nidhamu ya matumizi ya fedha kwa hiyo ni jukumu  la Baraza la Madiwani kusimamia na kuhakikisha kuwa mapato yote yanayokusanywa katika vyanzo vya ndani yanatumika ipasavyo.

Fikiri amesema kuwa ipo haja ya kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuhakikisha miradi ya maendeleo  inatekelezwa.

"Ni lazima Waheshimiwa Madiwani utaratibu wa kukagua miradi hiyo inayotekelezwa na Halmashauri kupitia kamati  zako, unafanyika mara kwa mara , Serikali inawekeza fehda nyingi katika miradi ili tuone matokeo chanya kuna haja kubwa ya kushirikiana kikamilifu na wataalamu w Manispaa kuhakikisha miradi inatekelezwa na wananchi wanapata hudma bora " Amesema Fikiri.

Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro , Christine Ishengoma, amewataka Madiwani kuhakikisha wanasimamia vyema fedha za miradi ili iwe na tija kwa wananchi.


1 comment:

  1. Nimeipenda hii lakini nidhamu ya fedha na maadili Kwa watumishi ndy MSINGI wa kuyafikia haya

    Pia kwenye utekelezaji wa mambo yanayowahusu jamii mfano masoko na stand ni vyema kushirikisha wausika wa miradi hiyo ili kuondoa migogoro pale inapokamilika na kuamuliwa kuamia wakagoma Kwa madai ya kutoshirikishwa

    ReplyDelete

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.