Header Ads

DIWANI KANGA AELEKEZA NGUVU UJENZI WA OFISI ZA MITAA KATA YA KILAKALA.

 

Diwani wa Kata ya Kilakala Mhe: Marco Kanga, akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Uwalimu Kata ya Kilakala.










DIWANI wa Kata ya Kilakala, Mhe: Marco Kanga, amesema kwa Sasa mkakati uliopo ni kuhakikisha kwamba kila Mtaa unakuwa na Ofisi ya Mtaa.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 10/2021 wakati wa mwendelezo wake wa Ziara ya kusikiliza na kutatua Kero za Wananchi wa Kata ya Kilakala.

Akizungumza na wananchi akiwa katika Mtaa wa Uwalimu Kata ya Kilakala, Kanga, amesema kumekuwa na changamoto ya Wananchi kufuata huduma Ofisi ya Kata Jambo ambalo limekuwa usumbufu kwa Wananchi wanaokaa maeneo ya mbali .

" Wananchi wengi wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma Ofisi ya Kata kwa Watendaji wao wa Mitaa, niwahakikishie kwamba nguvu nyingi nitaelekeza katika ujenzi wa Ofisi za Mitaa na nitajitolea fedha zangu kuchangia miradi hiyo, lakini tutafanya mashindano Mtaa utakaokuwa wa kwanza kukamilisha ujenzi huo tutawapatia zawadi tunahitaji sana michango ya Wananchi Serikali haiwezi kufanya vitu vyote peke yake lazima Wananchi wachangie" Amesema Kanga.

Katika hatua nyengine, Kanga, amewataka Wananchi kuendelea kuchangia miradi ya Maendeleo Kama vile miradi ya afya, barabara, vituo vya Polisi, Shule .

Amesema kuwa faida ya Wananchi kuchangia miradi hiyo ya Maendeleo ni Serikali kuweza kutoa huduma bora kwa Wananchi.

" Ukiangalia tumekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule zetu mfano Shule ya Sekondari Lupanga madarasa 4 yamekamilika hii yote ni ushirikiano wa Serikali na Wananchi, niwaombe sana Wananchi tushirikiane , sio Kama mtu ameshakuwa Diwani basi kila kitu afanye yeye lazima tuwe wamoja maana bila nyie hata hii nafasi yangu ya Udiwani nisingeweza kuipata" Ameongeza Kanga.

Katika upande wa afya, Mhe. Kanga, amesema ifikapo mwaka 2025 kwa kushirikiana na Uongozi wa Kata na Serikali , atahakikisha kwamba anafanya upanuzi wa Zahanati ya Kata kuwa Kituo Cha afya chenye kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Aidha, katika upande wa mitaro ya barabara ,amesema kuwa kwa wale ambao nyumba zao mbele zimepitiwa na mtaro basi jukumu lao ni kuona mitaro hiyo inakuwa misafi na anaisimamia.

Kuhusu miradi ya maji, amewashukuru MORUWASA kwa kuwapa mradi wa Maji wa Bong'ola na muda sio mrefu mradi wa Maji wa Bigwa Kisiwani utakuwa umekamilika na utawanufaisha walaji wengi.

Kwa upande wa mikopo ya Halmashauri, Kanga, amewataka wakina mama , Vijana na watu wenye ulemavu kutengeneza vikundi kwani Manispaa ya Morogoro inatenga asilimia 10 kupitia mapato yake ya ndani.

Aidha, amewataka Wafanyabiashara Wajasiriamali wote katika Kata ya Kilakala kuwa tayari kuupokea mradi wa Soko la Kilakala linaloelekea kukamilika na kuweza kujipatia fursa za kufanya biashara zao katika Soko lao na kuchangia uchumi wa Kata hiyo.

Kuhusu ulinzi na usalama, amesema atahakikisha kwamba Kata hiyo inajenga Kituo Cha Kisasa Cha Polisi ili kukomesha suala la uharifu na kuwafanya Wananchi wa Kilakala kuwa salama na kuendelea kufanya shughuli zao za uzalishaji mali kwa amani.

Hakuachilia mbali suala la michezo, ambapo amesema kufikia Agosti mwaka 2021 , ataanzisha mashindano ya michezo ikiwamo mpira wa miguu kwa Mitaa yote 15 iliyopo Kata ya Kilakala.

Mwisho amesema ataendelea kushirikiana na Wananchi wa Kilakala katika kuleta maendeleo kwa kufanya ziara mbalimbali za kusikiliza na kutatua Kero za Wananchi.

2 comments:

  1. Hongera sana Mh Diwani kwa kazi nzuri unayoifanya! Hakika sisi Kama Watendaji wa mitaa iliyopo kata ya Kilakala hatutokuangusha.

    ReplyDelete
  2. hongera sana Mh diwani pamoja na afsa mtendaji Mungu awabariki ili kuwatumikia wananch wa kilakala na kuwaletea maendeleo

    ReplyDelete

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.