Header Ads

HAKUNA SABABU YA KUSAFIRI UMBALI WA KILOMITA 50 KUJA WILAYANI KUFUATA HUDUMA , TUMIENI MTANDAO KUFANYA VIKAO NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI WENU-DC MSANDO.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, (wanne kutoka kushoto), akiwa pamoja na Maafisa Tarafa wa Wilaya ya Morogoro wakati wa kuwakabidhi Laptop.
                        

                        

                     

MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amesema hakuna sababu ya Mtendaji au mwananchi kusafiri zaidi ya Kilomita 50 kufuata huduma katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya badala yake wanaweza kuongea na Mkuu wa Wilaya kwa kupitia mtandao  (zoom Meeting) akiwa kwenye Tarafa yake.

Kauli hiyo ameitoa Julai 02/2021  ,mara baada ya kumalizika kwa tukio fupi la makabidhiano ya kuwapa Maafisa Tarafa Laptop 7 kwa ajili ya kuweza kuwahudumia wananchi pamoja na Maafisa hao kuweza kuandaa taarifa zao kwa kutumia Laptop hizo alizowapatia na kuzitumia kwa wakati.

Akziungumza na Waandishi wa habari, DC Msando, amesema  kuwa wananchi wengi sasa hivi hawahitaji kupita kwa wanaowazuia au kucheleweshwa kupata suluhu ya kero zao kwani tayari mazingira ya ufanyaji kazi kwa watendaji ameshayaimarisha .

"Wilaya yetu ya Morogoro ina jumla ya Kata 60, sio rahisi kufika katika Kata zote kwa wakati mmoja , mtandao utasaidia sana kuweza kutatua kero kwa haraka kuliko kusubiria kufika katika Ofisi ya Mkuu w Wilaya kwani wananchi wote katika Tarafa zao wataweza kuwasiliana moja kwa moja na mimi na tutawasikiliza , kwa sasa vikao vyetu tutatumia mtandao (zoom Meeting)  kati ya Maafisa Tarafa, Katibu Tawala wa Wilaya , Mkuu wa Wilaya na wananchi tumefanya majaribio na majaribio yetu yameonekana kwenda kuzaa matunda" Amesema DC Msando.

Akizungumza kwa niaba ya Maafisa Tarafa wote wa  Wilaya ya Morogoro , Afisa  Tarafa ya Mvuha, Fabius Byamungu amemshukuru  Mkuu wa Wilaya na kusema kuwa mfumo wa kutumia mtandao kwa kuwasilisha taarifa ndio mara ya kwanza kuanzishwa  katika Wilaya ya Morogoro huku akimuahidi kwenda kutumia Laptop hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na pamoja na kuweza kutatua kero za wananchi kwa haraka zaidi tofauti na awali .

Byamungu  ,amesema kuwa kutoka Tarafa ya Mvuha hadi Makao Makuu ya Wilaya ni Kilomita 78 hivyo kuanzishwa kwa mfumo huo kutawapunguzia umbali wa kusafiri kwa muda mrefu kuwasilisha taarifa au kufuata maelekezo.

" Tunampongeza sana Mkuu wetu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando ,  amekuja na mfumo mpya, hatukuwa na huu mfumo hii ni mara ya kwanza na ameandika historia mpya , tunamuahidi ushirikiano wa kufanya kazi kwa uwaledi mkubwa wa kuwatumikia wananchi pamoja na kutoa taarifa kwa wakati , tunaomba asiishie hapa azidi kubuni mbinu mpya wa watendaji wake ili kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuwatumikia wananchi " Amesema Byamungu.

Kwa upande wa Afisa Tehama Manispaa ya Morogoro, Kitutu Mshana, amewaomba  Maafisa Tarafa hao  kuzitumia Laptop hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa ili yaendane na malengo ya Mkuu wa Wilaya.

DC Msando, amekabidhi Laptop, 7 zenye thamani ya Tsh.880,000/= kwa kila moja kwa Maafisa Tarafa wote ikiwamo Tarafa ya Manispaa ya Morogoro, Mikese, Bwakila, Mkuyuni, Mvuha , Ngerengere  na Matombo.

  


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.