FAINALI YA NDWATA CUP YAFIKIA TAMATI, J.L ACADEMY WAIBUKA KIDEDEA.
Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako, (katikati) akisalimiana na wachezaji , (kulia) , Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Eng. Hamis Ndwata,
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, akizungumza na wanamichezo.
MASHINDAO ya Ndwata CUP 2021 yamefikia Tamati huku ikishuhudiwa Timu ya New J.L Academy ya Kihonda Maghorofani ikifanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kuibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 dhidi ya Ngerengere FC .
Fainali hiyo imefanyika Julai 04/2021 katika Uwanja wa mpira wa miguu wa Polyster Klabu uliopo Kihonda Maghorofani .
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ambaye pia ni Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako, amewataka wachezaji hao kuendelea kujitunza ili kulinda vipaji vyao.
Kipako, amesema kuwa ili vijana wewe kuendelea na vipaji vyao lazima wajilinde na kuepukana na vitu ambavyo vitachangia kuporomoka kwa viwango walivyo navyo.
"Tuneshuhudia mpira mzuri sana, marefarii wamefanya kazi kubwa wanasatahili pongezi ni wadogo lakini tunaamini watakuja kwa marefa bora sana hapa nchini, lengine ni vipaji tumeviona kikubwa ili wasiweze kuviendeleza lazima wajikinge na ngono zembe, ulaji wa vyakula vya mafuta , soda na starehe , kwa kufanya hivyo tutakuja kupata wachezaji wazuri sana kwani Morogoro imekuwa chuo cha kuzalisha wachezaji bora sana wanaoshiriki ligi mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu " Amesema Kipako.
Kipako, amempongeza Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Eng. Hamis Ndwata, kwa kuanzisha mashindo hayo huku akiwataka wadau na wananchi waweze kumuunga mkono.
Katika hatua nyengine,amewataka wachezaji hao wasiishie kwenye michezo bali mpira ni ajira hivyo watumie nafasi yao kama vijana kwa ajili ya kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotokana na Serikali hususani mkopo wa Halmashauri ambao hauna riba.
"Manispaa na Halmashauri zimekuwa zikitoa mkopo wa asilimi 10 ya mapato yake ya ndani, asilimia 4 Vijana, asilimia 4 Wanawake na asilimia 2 ya watu wenye ulemavu hivyo ni vyema wakajiunga katika vikundi ili wanufaike na mikopo hiyo lakini kikubwa uaminifu unatakiwa Vijana wengi wakipata pesa wanakimbia tofauti na wakina mama ambao tunawaona katika shughuli zao , Serikali yenu ina wajali lakini nasisi tuoneshe uaminifu katika hili " Ameongeza Kipako.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini , Fikiri Juma, amempongeza diwani huyo kwa kuanzisha ligi hiyo , ikiwa michezo kwa sasa inatoa ajira nyingi kwa vijana na kutoa wito kwa wanamichezo hao wajitume kwenye michezo hiyo, ili baadae wakacheze kwenye timu kubwa.
""Diwani kwa hili umefanya jambo jema sana, mimi mdau wa michezo naufahamu sana mpira, asilimia ya vijana niwaona hapa niwatu amabao wamepita katika mikono yangu, natumaini Morogoro katika siku za usoni tunaenda kurudisha heshima yetu katika michezo, Ilani imesema suala la michezo na umeitekeleza kwa kishindo, Chama kipo pamoja na wewe tunaamini huko mbele tutafikia sehemu nzuri sana " Amesema Fikiri.
Kwa upande wa Mdhamini wa michuano hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Eng. Hamis Ndwata, amesema lengo na madhumuni ya michuano hiyo ni kuinua vipaji vya vijana, kuimarisha umoja, kudumisha amani, pamoja kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mfano wa kuigwa kusaidia kuinua michezo hapa nchini.
"Michunao hii imeshirikisha timu sita za mpira wa miguu kutoka J.L Academy, Ngerengere FC , Kihonda Maghorofani FC , Usitambie Ujana FC , Moa Market , pamoja na Jamaica, tunashukuru sana timu shiriki kwa kufanikisha ndoto yangu hapa ni mwanzo hivyo tuna amni kwamba baadae tutakuwa na mashindo makubwa zaidi ya haya na changamoto zote zilizojitokeza tutazifanyia kazi " Amesema Eng. Ndwata.
Kwa upande wadau wa michezo walihudhuria katika michuano hiyo akiwamo Henry Joseph Shindika, wamemshukuru diwani huyo kwa kuanzisha Ligi hiyo ambayo imewapa moyo vijana hao wa kufanya mazoezi ili kuendeleza vipaji vyao, ambavyo hapo baadae vitakuja kuwapatia ajira na kuinuka kiuchumi.
Post a Comment