MANISPAA YA KINONDONI YAPONGEZA UTARATIBU WA SOKO KUU CHIFU KINGALU MOROGORO
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni , Mhe. Songoro Mnyonge, (wapili kutoka kushoto) akisalimiana na Mwneyekiti wa Soko Kuu la Chifu Kingalu (wapili kulia), Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Paschal Kihanga (kushoto), (kulia) Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Mohamed Lukwale.
MANISPAA ya Kinondoni wameipongeza Manispaa ya Morogoro pamoja na Uongozi wa Soko Kuu la Chifu Kingalu kwa utaratibu mzuri waliouweka katika Soko hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Songoro Mnyonge, Julai 02/2021 , katika ziara yao ya kujifunza kuendesha miradi ya kimkakati hususani Soko Kuu la Chifu Kingalu.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara hio, Mhe. Songoro, amesema utaratibu uliopo katika Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro wamefurahishwa nao huku akisema watahakikisha kwamba wanachukua uzoefu huo na kwenda kuufanyia kazi katika Soko lao.
Songoro,amesema kuwa , Soko likiwa na utaratibu ni rahisi sana kupelekea kutokuwepo kwa migogoro baina ya wafanyabiashara na Viongozi.
"Wenzetu mmetutangulia , tayari mnasoko kubwa na lenye vigezo , Soko lenu lina nafasi kubwa licha ya changamoto za hapa na pale bado tumeona ipo haja ya sisi kuja kujifunza ili tuangalie namna ya kuwapanga wafanyabiashara wetu, lakini kama kuna mapungufu tutayachukua na kuyarekebisha , tunaamini kwamba ziara yetu imekuwa na mafanikio makubwa na tumejifunza vingi sana " Amesema Songoro.
Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Paschal Kihanga, amepongeza Manispaa ya Kinondoni kwa hatua waliochukua kwani Manispaa ya Morogoro imekuwa chuo cha mafunzo hususani katika miradi ya kimkakati.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni , Stela Msofe, amefurahishwa zaidi na utaratibu mzuri kwa maeneo ya kuuzia na mgawanyo wa maeneo ya kuuzia kwa wafanyabiashara wote jambo ambalo linaepusha migogoro na migongano ambayo ingeweza kujitokeza kwa wafanyabishara hao.
Post a Comment