Header Ads

DIWANI KANGA ACHANGIA 50,000/= VIKUNDI VYA WAUZA MBOGA KILAKALA KUWAUNGA MKONO KATIKA KUONGEZA MITAJI YAO.


Diwani wa Kata ya Kilakala Mhe Marco Kanga akimkabidhi Kiongozi wa vikundi vya wauza mboga mboga Kilakala kiasi Cha Shilingi 50,000/=











DIWANI wa Kata  ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, amechangia kiasi cha shilingi 50,000/= kwa vikundi vya wauza mboga Kata ya Kilaka kwa ajili ya kuongeza mtaji.

Akizungumza na Wajasiriamali hao wa mbogamboga leo Julai 8/2021 , Kanga, amesema Wajasiriamali wanahitaji kutengenezewa Mazingira rafiki ili waweze kufanya biashara zao.

Kanga, amesewataka Wajasiriamali hao kuchangamkia fursa kwani Soko la Kilakala muda wowote linaweza kuanza kazi hivyo Ni fursa kwao kulitumia Soko lao walilokuwa wakisubiria kwa muda mrefu.

Amesema kuwa Manispaa ya Morogoro inatenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya Mkopo wa Vijana , Wanawake na Watu wenye Ulemavu , hivyo ni wakati muafaka wakujipanga ili fursa hizo ziwafikie.

" Nimefanya ziara yangu hapa , lakini nimeona wakina mama wanavyo chakalika , niwaombe Sana mtumieni Afisa Maendeleo ya Jamii awasaidie ili mpate Mkopo nikiwaangalia hapa wote mnakopesheka kikubwa Mara baada ya kupata fedha uaminifu unatakiwa ili kurudisha marejesho kwa wakati na wengine waweze kutumia Mkopo huo" Amesema Kanga.

Amesema kuwa, atahakikisha anatekeleza Yale yote aliyoyaahidi kwa Wananchi .

Diwani Kanga, amesema yupo mbioni kufanya ziara za kusikiliza na kutatua Kero za Wananchi kwa Mitaa yote, huku akiwataka Viongozi wenye dhamana kutowapuuza Wananchi na watoe huduma bora katika kuijenga Manispaa ya Morogoro.

Mwisho , ameupongeza Uongozi wa vikundi hivyo vya mboga mboga kwa jinsi walivyojipanga na wanavyoendesha biashara zao .

Ameahidi kushirikiana nao kuhakikisha Wajasiriamali wanatoka katika hatua ya Ujasiriamali kwenda hatua ya kuwa wafanyabiashara wakubwa.

Naye kiongozi wa vikundi vya wauza mboga mboga Kilakala, Maria Augastino, kwa niaba ya Wajasiriamali wenzake wamempongeza Diwani kwa kuwa karibu na Wajasiriamali hao.

" Zaidi ya miaka 5 sisi tumekuwa Kama yatima, leo tumempata Diwani ambaye anajali Wananchi wake, Wajasiriamali, tunamshukuru Sana aendelee na moyo wa kutusaidia, niwaombe Wananchi wenzangu tumuunge mkono Diwani wetu tufanye kazi uchaguzi imeisha Diwani mmoja tu, tunaamini fursa za Kilakala ni nyingi tunakuomba uzidi kutupambania" Amesema Mama Augastino.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.