RC SHIGELA AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII MKOA WA MOROGORO KUWA CHACHU YA ONGEZEKO LA BIMA YA iCHF KWA WANANCHI.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe.Martine Shigela, akifungua Mkutano wa Nusu Mwaka wa Tathimini ya Mkataba wa Lishe na Bima ya Afya ya Jamii (iCHF).
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Mariam Mtunguja,akizungumza na washiriki katika Mkutano wa Nusu Mwaka wa Tathimini ya Mkataba wa Lishe na Bima ya Afya ya Jamii (iCHF).
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kusirya Ukio (kulia) akizungumza na washiriki katika Mkutano wa Nusu Mwaka wa Tathimini ya Mkataba wa Lishe na Bima ya Afya ya Jamii (iCHF).
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabiri Makame, akitoa hoja.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Mhe. Ngollo Malenya, akijitambulisha.
Mratibu wa iCHF Mkoa wa Morogoro, Bi. Elisia Mtesigwa, akitoa taarifa ya tathimini ya mfuko wa Bima hiyo katika Mkutano wa Nusu Mwaka wa Tathimini ya Mkataba wa Lishe na Bima ya Afya ya Jamii (iCHF).
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amewata Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halamshauri zote zilizopo Mkoa wa Morogoro kusimamia kwa kasi ongezeko la Bima ya CHF iliyoboreshwa (iCHF) kwa Wananchi.
Hayo ameyazungumza leo Julai 16/2021 katika Mkutano wa Nussu
Mwaka wa Tathimini yaa Mkataba wa Lishe na Bima ya Afya ya Jamii (ICHF).
Akizungumza na waashiriki katika Mkutano huo, RC Shigela,
amesema zipo changamoto katika Mkoa wa Morogoro ambapo muitiko wa Wananchi
kukata Bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa .
RC Shigela, amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii wa
Halmashauri zote Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi kuona njia mbalimbali za kuongeza idadi ya wananchi katika mfuko wa
bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa.
Amesema kwa Mkoa wa Morogoro umefikia asilimia 9.4 ya zoezi la uandikishaji wa Bima za CHF iliyoboreshwa ambapo kwa malengo ya
kufikia mwaka 2025 Mkoa wa Morogoro unatakiwa kufikia asilimia 34%.
Amesema kuwa kati ya asiliia 9.4% za waliojiandikisha katika
mfuko wa Bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa ni asilimia3.4% ya wananchi
ambao ndio wanapata huduma ya bima ipasavyo.
‘’Bado Mkoa wetu wa Morogoro tunachangamoto kubwa ya bima
hii ya CHF iliyoboreshwa , asilimia ya wanachama wetu tuliowaandikisha
hawapati huduma kama inavyostahili, kumekuwa na malalamiko sana katika upande
huu wa bima, wengi wanalalamika dawa hakuna wakati sehemu nyengine zipo,
Maafisa Maendeleo nyie ni watu muhimu sana katika eneo hili, na mnajukumu hilo na ndio maana mmesomeshwa na
Serikali tupe huo utaalamu hakikisheni idadi ya wanachama wanaongezeka’’Amesema
RC Shigela.
Katika hatua nyengine, amepiga marufuku Watumishi katika
Vituo vya afya wanaotumia fedha za huduma zinazotolewa na wagonjwa Hospitalini
kuzifanya ni mali yao.
Amesema kuwa Katika Vituo vya afya kumekuwa na mchezo mchafu
ambao baadhi ya watumishi wamekuwa wakihudumia wagonjwa wasiokuwa na bima
kuchukua fedha bila kuingiza katika mfumo wa malipo.
‘’Nitoe rai kwaa waatumishi wa namna hiyo , utakuta baaadhi
ya Vituo vya afya idadi kubwa ya wanaohudumiwa wamekuwa wakiwaandikisha katika
matibabu ya huduma za msamaha , huku fedhaa zaa wagonjwa wakizitumbukiza mifukoni
, tutakao wabaini tutachukua hatua kubwa za kisheria , ni bora tubakie na
watumishi wachache kuliko kubaki na rundo la watumishi wanaotuhujumu’’Ameongeza
RC Shigela.
Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Mariam
Mtunguja, amewaomba wataalamu pamoja na wadau wa afya wasirudi nyuma kwani
suala la lishe linatakiwa lipewe kipaumbele.
Bi. Mtunguja, amesema kuwa tofauti kubwaa ya watoto
kupishana katika kiakili kinatokana na kupata lishe bora.
‘’Mtoto akipata virutubisho vya kutosha anakuwa na akili
nyingi, sasa ni jukumu letu kuhakikisha sualaa la lishe linakuwa agenda mama
katika vikao vyetu ili tutengeneze vizazi vyenye akili kwa ajili ya Mkoa wetu
wa Morogoro na Taifa kwa ujumla’’ Amesema Bi. Mtunguja.
Amesema kuanzia mwaka wa fedha wa bajeti ya 2021/2022 vipimo
vya utambuzi wa lishe vitaapimwa kuanzia ngazi ya Kata.
Katika Mkutano wa nusu mwaka wa Tathimini ya Mkataba wa
Lishe na Bima ya afya ya Jamii (iCHF) , ni pamoja na Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi wa Halmashauri, Wataalamu wa Halmashauri, Wataaalamu wa Lishe ngazi
ya Mkoa na Halmashauri pamoja na wadau wa lishe Mkoa na Halaamshauri zote.
Post a Comment