MHE. MABULA APIGA MARUFUKU WATENDAJI WA KATA, MITAA , NA WENYEVITI KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA VIWANJA NA ARDHI KATIKA MAENEO YAO.
NAIBU Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angeline Mabula, amepiga marufuku watendaji wa Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kutijihusha na uuzaji wa Viwanja na ardhi katika maeneo yao.
Kauli hiyo, ameitoa wakati wa Mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za migogoro ya ardhi Julai 13/2021 Mkoa wa Morogoro katika eneo la Stendi ya Dalala Mafiga Manispaa ya Morogoro .
Mhe. Mabula, amesema migogoro mingi ya ardhi inakuja kugundulika kuwa hata watendaji wa serikali wanahusika kutokana na kuwa mashahidi wa wanao nunua ardhi hivyo kukuza migogoro ya ardhi.
Amesema watendaji wa kata na Mitaa wanatakiwa kutatua kero za wananchi kwa kufanya mikutano ya hadhara katika Kata na Mitaa yao kwani watendaji wa Kata ndio walinzi wa amani katika kata zao.“ Ni marufuku watendaji wa Kata na Mitaa katika Manispaa kujihusisha na uuzwaji wa viwanja katika maeneo yenu au kuwa mashahidi ili kuepuka migogoro ya ardhi katika maeneo yenu.”Amesem Mhe. Mabula
“ Migogoro mingi inaweza kutatuliwa ngazi ya Kata ila kwakuwa hamtimizi majukumu yenu na kukwepa majukumu mnawaandikia wananchi barua na kuwaambia waende ngazi ya Manispaa na wilaya wakati uwezo wa kutatua migogoro kwa ngazi ya Kata mnayo, nataka kila mmoja atimize wajibu wake" Ameongeza Mhe. Mabula
Aidha, amewataka watumishi wote ngazi ya kata kuwa na mipango kazi inayotekelezeka na kufanya tathmini ya kazi zao ili kuweza kujipima.
Sentensi hiyo si sahihi. Poor kiswahili grammar.
ReplyDeleteSahihi ni ".... amepiga marufuku ......kujihusisha....." Sio amepiga marufuku kutojihusisha.
02. Muhimu zaidi angetuambia wanaonunua aridhi wakifika kwa wenyeviti wenyeviti waambieje, kwamba waende wapi....? that to give solution/an alternative.
03. Jambo lolote kwenye mtaa lisiposhuhudiwa na viongozi wa mtaa au kata bado kutakuwa na mgogoro tena. Ikiwa mwanasheria ataandikisha, atahakikisha vipi kuwa anachothibitisha ni halali?
Kwa kata au vijiji mbali na Manispaa hata wanasheria hakuna.Hakuna wakili wala mwanasheria wa kujitegemea,zaid ya mwanasheria wa manispaa/wilaya
ReplyDeleteHapo iko haja ya kutieleza mwananchi badala yakeaende wapi.
Kiuhalisia watendaji hawauzi maeneo au wenyeviti;bali ni mashahidi tu