Vijana watakiwa kuwa waaminifu katika kurejesha mikopo
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro , Enedy Mwanakatwe, (katikati) akizungumza na wanavikundi katika mkutano wa Vikundi vya mkopo Mtaa wa Bigwa Kisiwani Kata ya Kilakala.(kulia) Diwani wa Kata ya Kilakala , Mhe. Marco Kanga.
Diwani wa Kata ya Kilakala , Mhe. Marco Kanga, akizungumza na wanavikundi katika mkutano wa Vikundi vya mkopo Mtaa wa Bigwa Kisiwani Kata ya Kilakala.(kulia) Diwani wa Kata ya Kilakala , Mhe. Marco Kanga.
VIJANA wa Manispaa ya Morogoro wanaokopa mkopo wa asilimia 4 kutoka Halmshauri kuwa waaminifu kwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa juni 30/2021, na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro , Enedy Mwanakatwe, wakati akiwa katika mkutano wa Vikundi vya mkopo Mtaa wa Bigwa Kisiwani Kata ya Kilakala.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Mwanakatwe, amesema vijana wengi wanajuwa kuwa fedha za halmshauri ni ruzuku au sadaka ,nataka mtambue kuwa fedha hizo ni mkopo ambao kwa upendo wa Serikali umeweka masharti nafuu hivyo ninawataka vijana kurejesha fedha mlizokopa kulingana na mkataba uliowekwa ili zikawasaidie vijana wengine ambao hawajapata.
Aidha , Mwanakatwe, amewakumbusha wanavikundi kutunza kumbumbuku za biashara zao na kuwa waaminifu wao kwa wao.
Amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya baadhi ya vikundi kutokutunza kumbumbuku jambo ambalo linasababisha kushindwa kudhibiti mapato na matumizi ya fedha zao ikiwemo usomaji wa taarifa za vikundi.
Hata hivyo, amewahakikishia vijana na wanavikundi wote wa Manispaa ya Morogoro kuwa Serikali ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, iko bega Kwa bega kuhakikisha vijana na makundi mengine wanawezeshwa kiuchumi ili kuondokana na umaskini hivyo vijana na vikundi vyengine wanapaswa kuanzisha vikundi na kuvisajili katika maeneo yao kwa kufuata utaratibu na miongozo .
Pia ,amesema kuwa Manispaa ya Morogoro kupitia mapato yake ya ndani itaendelea kuhakikisha inawasaidia wananchi wake kuanzisha miradi mbalimbali vikiwemo viwanda vidogo vidogo na vya kati.
"Nipende kusema kuwa fedha zinazotolewa na Halmashauri sio sadaka na wala sio ruzuku ya Serikali,bali zinatakiwa kurejesha ili ziweze kukopeshwa kwa wengine, na zipo kanuni na sheria ziatafuatwa baada ya kushindwa kufanya marejesho, watakaohsindwa tutawafikisha Mahakamani kwa utaratibu uliopo , sasa leo tumekuja na kuwapa elimu tunakata tusifike huko lengo ni kuwasaidia wananchi wetu wajikwamue kiuchumi ,tuna zaidi ya vikundi 2900 vipo Manispaa na vinahitaji mkopo sasa lazima tuangalie vikundi vyenye vigezo kutokana na kanuni , sheria na utaratibu wa mikopo hiyo " Amesema Mwanakatwe.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Kilakala , Mhe. Marco Kanga, ameishukuru Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kufika kwao na kutoa elimu ya upatikanaji wa mkopo.
Kanga, amesema kuwa , atashirikiana kikamilifu na idara ya maendeleo ya Jamii ili kuona wananchi wa Kata ya Kilakala wananufaika na mkopo huo.
"Nimshukuru sana Dada yangu Mwanakatwe na timu yake, ujio wao umetufariji sana sisi wana Kilakala na Bigwa Kisiwani, tunaahidi kuendeleza ushirikiano baina ya Ofisi yangu ya Kata na Idara ya Mandeleo ya Jamii kuona ni kwa jinsi gani tunaweza kuwakwamua wananchi wetu kiuchumi na kupiga hatua " Amesema Kanga.
Kwa upande wake Afisa Vijana Manispaa ya Morogoro, Jackline Mushi, amesema wanaendelea kuwapatia vikundi vya vijana, elimu ya ujasiriamali sanjari na kuwawezeshaji kiuchumi.
Naye Catherine Mroso, amesema Idara ya Maendeleo ya Jamii ipo kwa ajili ya kuwasadia wananchi wote hivyo watahakikisha vikundi vyenye sifa na vigezo vinapatiwa mkopo ili kujikwamua kiuchumi.
Post a Comment