Header Ads

WAAJIRIWA WAPYA WAPATIWA SEMINA ELEKEZI KUHUSU UTUMISHI

 

DIVISHENI Divisheni ya Rasilimali watu na Utawala ya Manispaa ya Morogoro imetoa semina elekezi kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza utumishi wa umma kwa waajiriwa wapya wa Manispaa, walioajiriwa mwaka 2022 na mwaka huu 2023.

Katika semina hiyo iliyofanyika tarehe 18.09.2023 kwenye ukumbi wa mikutano wa Manispaa, waajiriwa wapya wamefahamishwa stahiki zao kama watumishi wa umma na baadae wakatambulishwa mfumo wa Mafunzo ya Wazi ya Masafa (ODel), unaowawezesha watumishi kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo utumishi wa umma.

Akizungumza wakati wa semina hiyo, Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu Manispaa ya Morogoro, Bi. Pilly Kitwana, amewasisitiza waajiriwa wapya kutimiza wajibu wao wakati wote ndipo waweze kudai haki zao.

“Hakuna haki bila wajibu. Watu wengine hupenda kudai haki zao wakati wao wanazembea ama hawatimizi wajibu wao. Hivyo ninapenda kuwaasa kwamba mtimize wajibu wenu ambao mnaupata katika ufafanuzi wa majukumu yenu (Job Discription) mliopewa na viongozi wenu, na maelekezo mengine ambayo yanapatikana kwenye miongozo mbalimbali ikiwemo Katiba ya Nchi, Standing Order na Ilani ya Chama Tawala kisha mtakuwa mnastahili kudai haki zenu” amefafanua  Kitwana.

Nao washiriki wa semina hiyo, ambao ni waajiriwa wapya wa kada mbalimba zikiwemo kada za Elimu, Afya,Dereva  na Watendaji wa Kata na Mitaa, waliahidi kutimiza wajibu wao kama watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni za maadili ya utumishi wa umma ili kuweza kutoa huduma bora kwa umma wa Morogoro.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.