RWAKATARE ATUMIA MCHEZO WA BAO KUAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO WILAYA YA GAIRO.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dkt. Rose K. Rwakatare,amewataka viongozi kutumia michezo mbalimbali katika kuhamaisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Kauli hiyo ameitoa Septemba 15/2023 katika ziara yake ya Kata kwa Kata Wilaya ya Gairo kuhamasisha uhai wa Jumuiya na kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rwakatare ,amewataka viongozi mbalimbali kutumia fursa ya uwepo wa michezo kwenye vijiji,mitaa,kata na tarafa kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Aidha,amesema kuwa kwenye kila mchezo kunakuwa na kundi kubwa la wananchi hivyo ni rahisi sana kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Hata hivyo,Rwakatare,amesema kuwa mchezo wa Bao la solo limekuwa kiunganishi kikubwa kwa wananchi na serikali kama ambavyo hayati mwalimu Nyerere alitumia mchezo huo katika harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika na kufaulu kuupata uhuru huo.
"Michezo yote inatakiwa inatakiwa kupewa kipaumbele sawa ili kuiweka jamii ya wanamichezo pamoja na kutumia fursa za michezo kwa maendeleo ya taifa, mchezo wa bao la solo ni mchezo ambao unachezwa na watu wa lika zote kwa ajili ya fursa na kutengeneza fursa za kimaendeleo wakiwa wanacheza mchezo huo" Amesema Rwakatare.
Pia, Rwakatare, amesema kuwa mchezo wa bao la solo umekuwa moja ya michezo ambayo unatakiwa kutumia akiri nyingi na maarifa kuliko kutumia nguvu hivyo ukicheza mara kwa mara mchezo huo akili yako itachangamka kwenye kufikiri.
Mwisho, amewaomba Vijana kuucheza na kuenzi mchezo huo wa kitamaduni kwa kuondoa dhana ya kuwa mchezo huo ni wawazee tu na sio mchezo wa vijana.
Dkt. Rwakatare,anaendelea na ziara hiyo katika Wilaya zote za Morogoro ili kuimarisha uhai wa Chama na kukagua miradi ya maendeleo ya Jumuiya na Serikali.
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
Post a Comment