DC NSEMWA AWAONYA WAFUGAJI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Rebeka Nsemwa, amewataka Wafugaji kuacha kujichukulia sheria mkononi pale wanapokutana na changamoto mbalimbali, hasa za kutuhumiwa kulisha mazao kwenye mashamba ya Wakulima.
Hayo ameyasema Septemba 18/2023 akiwa katika Mkutano wa kusikiliza kero za Wananchi wa Kijiji cha Seregera "B" Tarafa ya Mikese.
DC Nsemwa,amewataka wafugaji na wakulima hao kuishi kwa amani na kutojihusisha na migogoro inayoepukika kati yao na Wakulima, kwani migogoro hiyo inaondoa amani na utulivu mara inapotokea katika maeneo yao.
Katika hatua nyengine, DC Nsemwa kupitia Ofisi yake, ametoa pole mmoja wa wakulima aliyempoteza mtoto wake aliyevamiwa na wafugaji na kushambuliwa hadi kupoteza maisha.
"Vitendo hivi havikubariki katika jamii, hususani katika Serikali yetu inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan, Serikali imekuwa ikisisitizia amani kila siku, nitoe rai ni marufuku na ni kinyume cha sheria mtu yeyote kujichukulia hatua za kisheria mkononi" Amesema DC Nsemwa.
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
Post a Comment