Header Ads

KATA YA MAFIGA WAADHIMISHA SIKU YA USAFI DUNIANI.


KATA ya Mafiga Manispaa ya Morogoro imeadhimisha  siku ya usafishaji Duniani kwa kufanya usafi katika soko la zamani Manzese lililopo Manispaa ya Morogoro.

Maadhimisho hayo ya Kata yameongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Thomas Butabile kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Mafiga Septemba 16/2023.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo, Mhe. Butabile, amesema  kuwa kata ya Mafiga kufanya usafi  ni wajibu kwa kuwa kila mwisho wa mwezi lazima wafanye usafi ili kuepukana na mlipuko wa magonjwa.

 "Leo tumeadhimisha siku ya Usafishaji Duniani, kila mwananchi ana wajibu wa kushiriki kufanya usafi katika eneo lake linalo mzunguka, nitoe wito kwa wananchi wa Mafiga  kkufanya suala la usafi kuwa ni agenda yetu iwe kweney mikutano au nyumbani kwetu "Amesema Butabile.

Butabile, amewashukuru wananchi wote waliojitokeza katika  maadhimisho hayo huku akiwataka watimize wajibu wa kulipa ada ya taka ili Kata hiyo iwe safi na salama.

Mwisho, Mhe. Butabile, amesema sualala usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja na kuwataka wananchi kuendelea kutunza mazingira yanayowazunguka iwe ni nyumbani ama katika maeneo yao ya biashara.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Usafishaji Duniani 2023  “Kujifunza kupanga na Kuhimiza Uimarishaji Huduma za Udhibiti wa Taka" 

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.