DIWANI LUKOBE AGAWA JEZI MITAA 8 KWAA AJILI YA MAANDALIZI YA MBILINYI CUP OKTOBA 2023
DIWANI wa Kata ya Lukobe, Mhe. Selestine Mbilinyi, amegawa Jezi Seti moja kwa Mitaa 8 iliyopo Kata ya Lukobe kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Mbilinyi CUP linalotarajiwa kufanyika Oktoba 1/2023.
Ugawaji wa Jezi huo umefanyika Septemba 08/2023 katika Uwanja wa Tushikamane Shule ya Sekondari ikiwa ni maandalizi ya Kombe hilo.
Katika hafla hiyo ya kugawa jezi iliambatana na mchezo wa mpira wa miguu kati ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Viongozi wa Serikali Kata ya Lukobe dhidi ya Timu ya Mpira ya Miguu ya Chama Cha Mapinduzi CCM ikiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na Chama Tawala CCM.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi Jezi, Mhe. Mbilinyi ,amesema jezi hizo ni maandalizi ya Kombe la Mbilinyi CUP ambalo Bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa Ng'ombe, Mshindi wa Pili Jezi na Mshindi wa 3 Mpira.
Pia katika Ligi hiyo, kutakuwa na michezo ya Netball kwa wanawake ambapo Bingwa atazawadiwa Mbuzi.
"Ligi yetu itakuwa na Timu 8 kutoka kila Mtaa, tumeona tuje na mfumo mwengine, watu washazoea makombe yetu ambayo tumekuwa tukiyafanya lakini hii ni Ligi kabisa itakayoshirikisha Timu zote za Mitaa ya Kata ya Lukobe" Amesema Mbilinyi.
Kuhusu Mchezo wa CCM na Viongozi wa Serikali ambao ulimalizika kwa CCM kuibuka na magoli 3-0 dhidi ya Timu ya Viongo wa Serikali, amesema mchezo huo ulikuwa mahususi kwa ajili ya kujenga mahusiano baiana ya Chama na Serikali kwani wote wanawajibu wa kuhakikisha Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 inatekelezwa kwa asilimia 100 chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mbilinyi ,amesema mashindano hayo ya Mbilinyi CUP yanalenga kuibua vipaji vya michezo na kuipata wachezaji bora ambao wataonekana na kupata timu kubwa kwa ajili ya maisha yao.
"Katika Kata yangu kumekuwa na michezo mbalimbali ikiwa inafanyika, Kata yangu Vijana wengin wanapenda mpira wa miguu , kikubwa zaidi nimebaini kuwa kuna vijana wengi wanavipaji vya michezo lakini hawaendelezwi jambo ambalo limekuwa likisababisha vipaji vingi kupotea.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lukobe, Ndg. Aristotle Nikitas ,amesema mchezo wao umekuwa ni wa kiungwana sana na umewafanya Chama na Serikali kuongeza zaidi mahusiano ya kiutendaji wa kazi.
"Nampongeza Diwani wetu Mbilinyi, amebuni kitu kikubwa sana , kwanza kugawa jezi kwa Mitaa yetu ni kitu kikubwa chenye kudhamiria kuinua michezo Lukobe, lakini sisi kama Chama tutaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa Serikali yetu ili watekeleze kwa asilimia kubwa Ilani ya CCM katika kuwatumikia wananchi" Amesema Aristotle.
Post a Comment