Header Ads

BARAZA LA WATOTO MANISPAA YA MOROGORO LAKAMILISHA SAFU YA UONGOZI

 



BARAZA la watoto Manispaa ya Morogoro   limefanya uchaguzi wa kukamilisha safu ya Viongozi wataliongoza Baraza hilo kwa mwaka 2023.

Uchaguzi huo umefanyika Septemba 27/2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimo Manispaa ya Morogoro 

Uchaguzi huo wa viongozi ulienda sambamba na utoaji wa maada ya mwongozo wa uundaji wa Mbaraza katika ngazi ya Mitaa hadi Taifa pamoja na elimu ya ukatili dhidi ya watoto uliotolewa na Taasisi ya ZUIA TRAFIC TANZANIA.

 Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa kuwapata viongozi hao, Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro ambaye ndiye mgeni rasmi , Catherine Mrosso, amesema nafasi zilizogombewa ni pamoja na  Katibu,Katibu Msaidizi pamoja na  Mtunza Hazina.

Mrosso amesema kuwa baraza la watoto linajukumu la kutambua haki za watoto na kuzisimamia haki hizo na kutafuta njia za kuondoa changamoto zinazosababisha watoto kutotendewa haki zao na jamii.

Aidha, Mrosso,ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa baraza la watoto ili liweze kufanya kazi yake bila vikwazo kwa maendeleo ya watoto ambao ni taifa tegemewa la kesho.

Naye mratibu wa Dawati la Watoto Manispaa ya Morogoro, Joyce Mugambi, amewashauri watoto  hasa wa kike kuacha tamaa ambazo zinawaingiza kwenye matatizo yanayosababisha kupata mimba za utotoni ambazo zinaharibu malengo yao.

Mugambi, amewataka wazazi kuwalinda watoto wao ili wasiingie kwenye vishawishi hasa wanapokuwa shuleni kwani vishawishi hivyo ndivyo vinapelekea wao kushindwa kuendelea na masomo,

Katika uchaguzi huo , Vanessa Michael ameshinda nafasi ya Katibu kwa kupata kura 10, Glory Samson amepata kura 6 kuwa Kaimu Katibu , Happines Karimu ameshinda nafasi ya mwekahadhina kwa kupata kura 15 kati ya kura 20 zilizopingwa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.