CAMFED KUNUFAISHA SHULE ZA SEKONDARI MANISPAA MOROGORO KUPITIA MRADI WA ELIMU YA STADI ZA MAISHA
WANAFUNZI wa Shule za Sekondari Manispaa ya Morogoro wanatarajia kufikiwa na mradi wa Elimu ya Stadi za Maisha ambazo zitaendeshwa Shuleni zenye lengo la kuwasaidia wanafunzi kufikia malengo yao.
Akizungumza juu ya Mradi huo, Meneja miradi CAMFED kutoka Mkoa wa Morogoro, Latifa Sabuni ,amesema kuwa nia na madhumuni ya mradi huo ni kuwasaidia wanafunzi walioko shuleni kujisaidia kujitambua, kujijua wao ni nani na wanatakiwa kufanya nini, ili kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea.
Aidha,amesema kuwa mradi huo utawafikia Shule zote za Sekondari Manispaa ya Morogoro.
Latifa,amesema mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri 32 nchini.
"Mradi wetu utakuwa na tija kubwa kwani inalenga kuwasaidia wanafunzi hao kuweza kumaliza masomo yao, kuwafuatilia wanafunzi walioacha shule kuwashauri na kuwatia moyo ili warejee shuleni na kuendelea na masomo yao, wawezeshaji wa wanafunzi katika mradi huo hawaishii shuleni pekee lakini hata kuwasaidia kiushauri na mwongozo wanafunzi wanaopata changamoto mbalimbali katika jamii."Amesema Latifa.
Hata hivyo,amesema kuwa wapo wanafunzi watoro ambao wanapowatembelea majumbani na kuzungumza nao kirafiki huweka wazi sababu ya wao kutokuja shule, ambapo ni kuchangiwa na changamoto za kifamilia na tunapofanikiwa kuzitatua mwanafunzi huwa anarudi shuleni na kuendelea na shule kama wenzake.
Kwa upande wa Kaimu Afisa Elimu Sekondari, Anna Lupiano,amesema Manispaa inaunga mkono moja kwa moja mradi huo ambao unalenga kuwajengea uwezo wanafunzi ili kutambua changamoto zao na namna ya kukabiliana nazo.
"Kupitia programu hii, wanafunzi wetu watajifunza mada mbalimbali ambazo zinawafanya wao waweze kujitambua, kutambua changamoto zao wanazokumbana nazo katika mazingira ya kila siku, wito wangu kwa Waalimu Wakuu wa Shule wakaanze haraka kutekeleza mpango huu" Amesema Lupiano.
. JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia, bila ya kuingia website
Post a Comment