Header Ads

NGUVU YA WANANCHI YAKIMBIZA UJENZI WA MABOMA 4 NA OFISI 2 ZA WAALIMU SHULE YA MSINGI MISUFINI B.

 






WANANCHI wa Mafiga kwa kushirikiana na Uongozi wa Kata ikiwamo Wenyeviti wa Mitaa wamefanikiwa kunyanyua maboma 3, Ofisi 2 za Waalimu na Maktaba 1 katika Shule ya Msingi Misufini B.

Akizungumza juu ya Maboma hayo, Diwani wa Kata ya Mafiga Mhe Thomas Butabile, amewapongeza Wananchi na Viongozi wa Kata, Chama  na Mitaa kwa ushirikiano mkubwa wa kukamilisha ujenzi huo.

Butabile amesema Kata hiyo wamekuwa wakitekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa katika sekta ya Sekondari na Msingi.

"" Huu sio ujenzi wetu wa kwanza kwa kutumia nguvu ya Wananchi, tulianza kujenga maboma  4 Shule ya Msingi Mafiga B na Ofisi 1 ya Mwalimh Mkuu, tukajenga maboma 3 Shule ya Sekondari Mafiga na Maktaba na Jengo la Utawala , Ujenzi uzio na madarasa Misufini A na Sasa tumehamishia nguvu Misufini B " Amesema Butabile.

Aidha, amesema mara ujenzi wa maboma unapokamilika kazi ya upauaji ni ya Mkurugenzi wa Manispaa.

Mwisho, amewaomba Wananchi wa Kata hiyo, waendelee na ushirikiano huo huo hata katika miradi mingine ili kuleta Maendeleo ya pamoja ya Kata hiyo.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia, bila ya kuingia website


Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media...

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.