Header Ads

Ukijipandisha kwasababu ya uteuzi hutowatumikia watu-Rais Samia

 

Rais Samia amewataka viongozi kuwajibika, kuwatumikia watu na kuwa mabadiliko yaliyofanywa si adhabu, ni mabadiliko ya kawaida katika kuimarisha maeneo mabalimbali.

Rais Samia ameyasema hayo katika hafla ya kuwaapisha mawaziri na makatibu wakuu Ikulu ndogo Zanzibar.

''Ninachotarajia kwenu ni commitment kwenye kazi zenu, nyinyi ni watumishi, sisi ni watumishi wa watu sasa kuna mwingine akipata uteuzi anajiona sasa eeeh...atanijua mimi ni nani kwa hivyo sisi ni watumishi wa watu''.

Amewataka viongozi hao kuwa katika hali ya utulivu kabla ya kutoa maamuzi ya masuala mbalimbali

“Katika utumishi wa watu mahusiano ni jambo zuri sana. Sasa ukijipandisha unataka kukaribia mbinguni kwamba umepata uteuzi, hutowatumikia watu.” Alisema Rais Samia.

Katika mabadiliko aliyoyafanya, aliyekuwa waziri wa Madini, Dotto Biteko ndiye Naibu Waziri Mkuu, akihusika na urantibu wa shughuli za serikali, pia anakuwa waziri mpya wa Nishati.

Mara ya mwisho wadhifa wa Naibu waziri Mkuu ulikuwepo 1995 na kushikwa na Augustino Mrema wakati wa awamu ya pili ya uongozi wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Moja ya mabadiliko aliyoyafanya Rais Samia ni kuifuta Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, badala yake aliunda wizara nyingine mbili wizara ya Ujenzi na wizara ya Uchukuzi kama zilivyokuwa wakati wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.